****************************
07/07/2021 DAR ES SALAAM
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga kutoa elimu zaidi kwa wananchi hatua ambayo itawasaidia kutambua na kufahamu viashiria vya kihalifu kwenye maeneo yao
IGP Sirro amesema hayo leo alipotembelea banda la Polisi katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa Sabasaba na kufanya tathimini ya namna Jeshi hilo lilivyojipanga hasa kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo sambamba na maeneo mengine.
Naye Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Shirika la Uzalishajimali la Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Beatus Sila ameeleza namna shirika hilo lilivyojidhatiti katika kuhudumia wananchi hususani katika miradi yake ya kutoa mafunzo mbalimbali hasa yale ya umahiri wa kutumia bunduki za kiraia pamoja na miradi mingine inayotekelezwa na shirika hilo.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi kutoka kikosi cha Polisi Wanamaji Hassan Nyangali amesema Kikosi hicho kimejipanga katika kuwaelimisha wananchi kutoa taarifa hasa pale wanapoona ama kushuhudia watu au kikundi cha watu wakitekeleza uvuvi haramu kwenye ukanda wa bahari, maziwa pamoja na mito.