Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akihutubia wananchi wa kata ya Nyamhongolo katika viwanja vya shule ya msingi Nyamadoke kutoa mrejesho wa Bunge la bajeti lililoisha hivi karibuni na kusikiliza kero za wananchi.
Wananchi wa kata ya Nyamhongolo waliojitokeza kusikiliza mrejesho wa bajeti na kutoa kero zao Kwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula aliyeambatana na wataalamu wa idara mbalimbali za manispaa ya Ilemela
………………………………………………………
Kiasi cha shilingi bilioni kumi na nane na milioni mia mbili na kumi na tatu kimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021-2022 kwaajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya kata ya Nyamhongolo
Akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika viwanja vya shule ya msingi Nyamadoke, Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu waziri wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa kata ya Nyamhongolo imetengewa fedha nyingi kuliko kata yeyote kwa jimbo la Ilemela kwa mwaka huu wa fedha ambapo kiasi cha shilingi bilioni kumi na mbili kimetengwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya mboga mboga kupitia nyamadoke kuelekea nyamhongolo yenye urefu wa kilomita tisa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa majiji TSCP, milioni arobaini na mbili zikitegemewa kukamilisha jengo la kutolea huduma za mama na mtoto kwa zahanati ya Nyamhongolo, milioni hamsini kwaajili ya kukamilisha zahanati ya nyamadoke, milioni tisini kwaajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara huku bilioni sita zikitarajiwa kukamilisha ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi na malori nyamhongo 4833 Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akifafanua juu ya miradi mbalimbali ya Maendeleo itakayotekelezwa ndani ya kata ya Nyamhongolo kwa mwaka wa fedha wa 2021/20212
‘.. Ukiangalia kwa haraka haraka nyingi mmetengewa fedha nyingi sana za maendeleo, Haya kwenye sekta ya umeme mmepewa transfoma saba zenye KVA 100 na zenye KVA 200 zipo sita, Mungu awape nini? ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula akawataka wananchi hao kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hasan na Serikali yake ya awamu ya sita ili kuzidi kuwatumia na kuwaletea maendeleo sambamba na kuwasisitiza kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoitesa dunia kwa sasa
Akimkaribisha Mbunge huyo, Afisa tarafa wa wilaya ya Ilemela Ndugu Godfrey Mzava mbali na kufikisha salamu za mkuu wa wilaya ya Ilemela Ndugu Hassan Masala kwa wananchi akamhakikishia kuwa wilaya ya Ilemela iko salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo huku akiwasisitiza wananchi wote kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya uharifu kwa viongozi wa maeneo yao au katika vyombo vya ulinzi na usalama ili wilaya hiyo iendelee kuwa salama
Nae mwakilishi wa mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni Afisa ardhi na mipango miji wa wilaya hiyo, Ndugu Shukrani Kyando akafafanua kuwa manispaa ya Ilemela inaendelea na utatuzi wa kero na changamoto zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo na ya kimkakati
Aidha katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula ameongeza kuwa wakati wa uchaguzi chama chake kilinadi Ilani ya uchaguzi na wagombea wake hatimae wananchi wakakiamini na kuchagua wagombea wa CCM, Hivyo kilichobaki ni kutekeleza kile walichokiahidi kupitia Ilani hiyo bila kujali tofauti za kiitikadi ya vyama ili kuharakisha utekelezaji wa maendeleo kwa wananchi
Akihitimisha moja ya wananchi waliohudhuria mkutano huo Ndugu Aron Samuel akampongeza Mbunge huyo kupitia idara ya ardhi kwa namna idara hiyo ilivyobadilika na kushughulikia kero za wananchi kwa haki, usawa na haraka bila kujali hali zao za kimaisha