Home Mchanganyiko RAIS MHE.DK. MWINYI AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

RAIS MHE.DK. MWINYI AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi wakati wa Meneja Mkuu wa Hoteli ya Riu Palace Zanzibar Ndg.Hamad Zaied akimkabidhi Komputa kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Chaani Bi.Latifa Masoud Issa, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Madarasa manane mapya ya Skuli hiyo yaliojengwa na kukamilika kwa ajili ya Wanafunzi wa Skuli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Chaani baada ya kuyafungua Madarasa manane mapya ya Skuli hiyo, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kaskazinin Unguja na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Chaani Wilaya ya Kaskazini “A”Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa Madarasa mapya manane ya Skuli hiyo.(Picha na Ikulu)

WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi ya Chaani Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) baada ya kuwafungulia rasmin madarasa yao mapya manane ya Skuli hiyo.(Picha na Ikulu)