Home Mchanganyiko MAKAMU WA RAIS AMFARIJI NAIBU GAVANA WA BENKI KUU

MAKAMU WA RAIS AMFARIJI NAIBU GAVANA WA BENKI KUU

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa naibu Gavana wa Benki kuu Dkt. Yamungu Kayandabila kufuatia kifo cha mama wa Naibu Gavana huyo Bi. Paulina Nkeyenge Kayandabila. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Bi Mbonimpaye Mpango.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Yamungu Kayandabila alipofika kumfariji kufuatia kifo cha Mama wa Naibu Gvana huyo kilichotokea Julai 04, 2021.

………………………………………………………………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amefika nyumbani kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila kuwafariji kufuatia kifo cha mama wa Naibu Gavana huyo  Bi.  Paulina Nkeyenge Kayandabila Aliefariki Julai 4 2021.

Makamu wa Rais akiongozana na Mkewe Bi Mbonimpaye Mpango amewafariji wafiwa hao na kuwaomba kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao. Makamu wa Rais amewashukuru wote waliojitokeza katika kuifariji familia hiyo na kuwaomba kuendelea kuwa na umoja na mshikamano hasa wanapopitia matatizo mbalimbali.