Home Mchanganyiko PACT TANZANIA ILIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA VIJANA

PACT TANZANIA ILIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA VIJANA

0

Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Mhe. Ng’wilabazu Lugigija (wa pili kutoka kulia) akipewa ufafanuzi na Shirika la Pact Tanzania kuhusu utekelezaji wa miradi yao hapa nchini.

************

Shirika la Tanzania Pact wamefanikiwa kuwapatia vijana takribani 9,595 ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi na zana za kujiongezea kipato pamoja kufanya juhudi kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo.

Ufadhili huo umetolewa katika nchi zaidi ya 35 duniani ambapo kwa hapa nchini shirika hilo limetimiza miaka 50 kupitia utekelezaji wake wa miradi ya USAID wa kizazi kipya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Pact Tanzania, Mariana Balampama, ameiomba TAMISEMI kuwasaidia vijana wao ili wapate kandarasi kupitia miradi mbalimbali mbali inayotekelezwa katika halmashauri zote nchini.

“Tayari wapo vijana walioweza kupata mafunzo katika fani za ufundi magari, ushonaji , upambaji na fani zingine”

Amesema kuwa ni furaha vijana wanaondoka na nyavu na manoari kwa ajili ya kwenda kavua bahari ya mbalimbali.

Bw. Francis Pirimin Komba ambaye ni Mratibu wa Mafunzo ya Uanagenzi Pacha aliye Mwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt.Pancras Bunjulu, amesema kwa sasa kuna vyuo zaidi ya 40 hapa nchini, wote wakikengewa stadi ya maisha.

“Sehemu ya kujifunza ujuzi ni sehemu nzuri katika maono ya maendeleo ya vijana sisi tunatoa ujuzi katika fani zaidi ya 90, wajitokeze ambapo kwa sasa kuna vyuo 25 vinakwenda kujengwa vijijini” amesema Komba.

Katika kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi ; mradi wa ACHIVE umetoa viti 156, makabati ya chuma 1033 pamoja na zana mbalimbali za kukusanyia taarifa.

Shirika hilo waliweza kufanya makabidhio ya vifaa ambapo ofisi ya jijini la Dar es Salaam iliwakilisha maeneo ya halmashauri zote nchini juu ya makabidhiano hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Ng’wilabazu Lugigija amelipongeza Shirika hilo lisilo la kiserika .

“Nalipongeza harakati na mikakati yao kwani wamekuwa kichocheo cha kukuza uchumi kwa kuzingatia maendeleo” amesema Ludigija.