Home Mchanganyiko WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MFUMO UTAKAOWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO...

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MFUMO UTAKAOWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO KWA NJIA YA KIDIGITALI

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi, ujulikananao kama SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU). Kulia kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi na kushoto kwake ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akijiandaa kubonyeza kitufe ili kuzindua rasmi mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi ujulikanao kwa jina la SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU). Kulia kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa    kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kuzindua rasmi mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi ujulikanao kwa jina la SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU) uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi kabla ya uzinduzi wa mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi ujulikanao kwa jina la SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU) uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Mwonekano wa mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi ujulikanao kwa jina la SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU) uliozinduliwa leo June 29,201 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa na baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi wa mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumishi na wananchi ujulikanao kwa jina la SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI (SWU) uliofanyika  leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akionyesha jarida la Utumishi Habari na Matukio mara baada ya kuzindua jarida hilo . Kulia kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi akishiriki uzinduzi wa jarida hilo na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa amezindua mifumo rasmi itakayowezesha watumishi wa umma na Wananchi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kutoa malalamiko, mapendekezo, ushauri, maulizo na pongezi moja kwa moja kwa njia ya kidigitali.

Akizindua mfumo huo leo June 29,2021 jijini Dodoma, Mhe Mchengerwa amesema, uzinduzi wa mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na wananchi.

Mchengerwa amesema mfumo huo unajulikana kwa jina la ‘Sema na waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora’ ambao unapatikana kwenye tovuti ya www.swu.utumishi.go.tz.

Amesema mifumo hiyo itakuwa miwili ambapo mmoja utatumiwa na watumishi na Wananchi ambao wanaishi maeneo yenye mawasiliano ya mtandao na mwingine ni kwa ajili ya watumishi ambao wapo katika maeneo ambayo hayana mawasiliano ya mtandao.

Hata hivyo Mchengerwa amefafanua kuwa kupitia mfumo huo mtumishi anaweza kutuma malalamiko yake akiambatanisha na nakala za barua zake kupitia mfumo huo ambao utamuwezesha yeye kuona malalamiko hayo moja kwa moja na kuweza kutoa maagizo au maelekezo lakini pia anaweza kuwasiliana na mtoa malalamiko moja kwa moja.

Mchengerwa amesema mfumo huo utarahisisha utendaji kazi, utawaondolea gharama Wananchi na watumishi ambao awali walilazimika kutumia gharama kubwa kutoka katika maeneo yao mpaka kufika Dodoma ambako ndio makao makuu ya ofisi ya Utumishi lakini pia utasaidia kuokoa muda.

Pia amesisitiza  kuwa wizara yake itachukua hatua kwa maofisa Utumishi wote ambao hawakuwasilisha taarifa za watumishi waliopaswa kupandishwa madaraja hivyo kusababisha watumishi hao kutopandishwa madaraja kutokana na uzembe wao.

Aidha, Mchengerwa amezindua Jarida la Utumishi la Habari na Matukio ili kuuhabarisha umma namna Ofisi yake inavyomsaidia Mhe. Rais kutekeleza jukumu la usimamizi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, jarida hilo litauhabarisha umma juu ya mafanikio ya Serikali yanayopatikani na utekezaji wa majukumu kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala Bora. 

“Jarida hili litakuwa linatoka kila baada ya miezi mitatu na litakuwa na maudhui ya utekelezaji wa maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa na matukio mbalimbali ambayo ofisi imekuwa ikiyafanya kwa masilahi ya umma hapa nchini,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, amefarijika kuona utekelezaji wa maelekezo ya kuanzishwa kwa mfumo wa ushughulikiaji wa malalamiko ya watumishi na wananchi umekamilika.

Naye  Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro amempongeza Mhe. Mchengewa kwa kuwahamasisha watendaji wake kutekeleza majukumu kwa njia ya kidijitali ili kurahisiha utoaji wa huduma kwa Watumishi wa Umma na wananchi.

“Mfumo huu wa SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI ni zao la hamasa yako ya utatuzi wa changamoto za watumishi na wananchi zitakazowasilishwa kupitia mfumo huo”, Dkt. Ndumbaro amesema