Home Mchanganyiko WADAU WA USAFIRISHAJI NCHINI WAFURAHISHWA NA HATUA YA SERIKALI KUPUNGUZA KERO BANDARINI

WADAU WA USAFIRISHAJI NCHINI WAFURAHISHWA NA HATUA YA SERIKALI KUPUNGUZA KERO BANDARINI

0

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Bw.Elias Lukumay akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Bw.Elias Lukumay (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam

Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw. Elitunu Mallamia akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini  Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

Wadau wa Usafirishaji nchini wameiomba Serikali kuingilia kati sheria inayopendekezwa nchini Zambia inayotaka asilimia 50 ya mizigo kutoka nchini ibebwe na raia wa nchi hiyo pekee, kwa kile walichokisema kuwa inaleta upinzani badala ya ushindani wa biashara kati ya Tanzania na Zambia. 
Akizungumza leo Jijini  Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Bw.Elias Lukumay, amesema Serikali ya awamu ya sita imeonyesha wazi kasi yake katika kutatua changamoto za usafirishaji bandarini.
“Tupo tayari kufanya biashara kwa ushindani lakini sio kwa ushindani wa sheria, hii itakomesha biashara za Watanzania ambao wamewekeza katika usafirishaji,”. Amesema  Bw.Lukumay.
Amesema miongoni mwa hatua muhimu na bora zilizochukulia na serikali katika kupunguza kero hizo ni pamoja na Katibu Mkuu Uchukuzi, kuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati majadiliano ya kusaka suluhu ya migogoro. 
Kwa mujibu wa Bw.Lukumay, kwa sababu hiyo ndiyo maana changamoto ya msongamano wa magari kuelekea bandarini imetatuliwa haraka. 
Aidha Bw.Lukumay amesema kuwa changamoto nyingine ni masuala ya forodha ambapo Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alikutana na wadau na kuzungumza nao hivyo kwa sasa wapo kwenye majaribu ya maboresho yaliyofanyika.
Pamoja hayo Bw.Lukumay amesema kuwa pamoja na mambo mengine, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu bandarini, mambo ambayo yatafanikisha kufikia hatua ya bandari ya Tanzania kubeba mizigo ya tani milioni 30 kwa wakati mmoja. 
Naye, Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw. Elitunu Mallamia, amesema hatua ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutatua changamoto za wadau wa usafirishaji ni muhimu na ina tija kwa taifa.
Amesema kwa sasa bandari inabeba takribani tani milioni 17 na kwa juhudi zinazofanywa kuna muelekeo wa kufikia tani milioni 30 siku zijazo.