Home Mchanganyiko TIC YAONGOZA KAMATI YA KUJADILI MASWALA YA MUWEKEZAJI DANGOTE

TIC YAONGOZA KAMATI YA KUJADILI MASWALA YA MUWEKEZAJI DANGOTE

0

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu I. Kazi Kushoto akipokea maoni toka kwa wajumbe wa kamati kutoka Wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki kikao hicho.

Wajumbe wa kamati kutoka Wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki kikao cha kujadili na kutoa maoni kuhusiana na maswala ya muwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote.

****************************

Taasisi za serikali na Wizara zilizopo kwenye kamati ya kujadili maswala ya muwekezaji wa Kiwanda cha saruji cha Dangote (Dangote Cement (T) LTD) zakutana na kujadili namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali za kiwanda hicho, kikao kazi hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Udzungwa kwenye ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarehe 23 Juni, 2021.

Kikao hicho ni muendelezo wa kikao cha Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey Mwambe na wawakilishi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichofanyika tarehe 8 Juni, 2021 ambapo Mhe. Waziri Mwambe alielekeza kuwa changamoto zilizopo kwenye kiwanda hicho cha saruji ziwasilishwe Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili waweze kuratibu kikao na wadau kwa ajili ya kukamilisha changamoto hizo na kutoa mapendekezo kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri wa Kisekta chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji.

Kutokana na muktadha huo Mkurugenzi Mtendaji wa (TIC) Dkt. Maduhu I. Kazi ameongoza kikao kazi hicho na kuelekeza kuwa kila taasisi ihakikishe inafanyia kazi makubaliano yaliyofikiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kutatua changamoto hizo.

Wadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jeshi la Polisi Tanzania (TPF), Dangote Cement (T) Ltd, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mawasiliano na Tehama na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA)