Home Mchanganyiko WAZIRI AWESO ATEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA KUHUSU USHIRIKIANO NA SERIKALI YA...

WAZIRI AWESO ATEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA KUHUSU USHIRIKIANO NA SERIKALI YA ZANZIBAR

0

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ,akizungumza kabla ya kusaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Maji na Nishati Mhe.Suleiman Masoud Makame kutoka Zanzibar ,akizungumza kabla ya kusaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar Dkt .Mngereza Mzee Miraji,,akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mwenzake wa Zanzibar Waziri wa Maji na Nishati Mhe.Suleiman Masoud Makame wakisaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya pande hizo mbili za Muungano hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mwenzake wa Zanzibar Waziri wa Maji na Nishati Mhe.Suleiman Masoud Makame wakionyesha mkataba baada ya kusaini makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya pande hizo mbili za Muungano hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zimesani makubaliano ya kutumia mfumo mpya wa teknolojia katika kutatua changamoto za maji baina ya pande hizo mbili muungano.

Makubaliano hayo yamefikiwa jijini Dodoma na Waziri wa maji Jumaa Aweso na Mwenzake wa Zanzibar Waziri wa Maji na Nishati Mhe.Suleiman Masoud Makame ikiwa ni baada  siku mbili  tu serikali hizo kuketi na kujadili kadhia za katika sekta ya maji na namna ya uboreshaji ikiwemo kutumia mifimo ya kiteknolojia.

Katika mazungumzo yao mawaziri hao wameweka bayana dhamira ya serikali ni kufikia malengo katika  kutataua changamoto za maji katika  Serikali ya mapinduzi Zanzibar na Tanzania bara.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema dhamira hiyo hiyo kutiliana saini makuabaliano ni kuhakikisha seriakli inamtua mama ndoa kichwani .

Wakati huo huo mawaziri hao wamezindua na kukagua moja ya mifumo hiyo mipya ambayo imeanza kufanya kazi katika majibio ya utoaji wa hudumua hiyo ya maji kwa wateja wake.

”Dhima ya serikali katika mfumo huo mpya inalenga kuhakikisha wateja wote wa huduma ya maji nhini wannaza kutumia huduma ili kuepuka malalaki ya kubabambikiziwa bili kubwa”amesema Mhe.Aweso

Katika mfumo huo zimetajwa sifa kadha ambazo zitamrahisishia mteja kupata huduma kwa haraka ikiwa ninpamoja mteja kununua maji kwa simu ya mkononi ,kuweza kuhama nyumba na unit,na kumhamishia mteja mwingine unit za maji,na kutambua kiwango cha maji yanayotumika kupitia simu ya mkononi.

”Makubaliano hayo yanalenga kutoa fursa kwa wizara hizo mbili zenye dhamana ya  kutoa huduma ya maji  kushirikishana uzoefu na mbinu mbalimbali ili kulifikia lengo la kufikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wananchi”

Naye Waziri wa Maji ,Nishati na Madini Zanzibar Seleman Masooud amesema kwa milango iko wazi kwa upande wa zanzibara watendaji wa Tanzania bara kwenda zanazibar ili kuongeza ufanisi mkubwa katika katika sekta maji.