Home Mchanganyiko WAZIRI KABUDI: ‘MAWAKILI TOENI TAARIFA OFISI YA WAKILI MKUU MSISUBIRI MPAKA MAMBO...

WAZIRI KABUDI: ‘MAWAKILI TOENI TAARIFA OFISI YA WAKILI MKUU MSISUBIRI MPAKA MAMBO YAWE MAGUMU’

0

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza  na washiriki wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,akisisitiza jambo kwa washiriki wa  Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiri wakifatilia hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma 

Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa Paramagamba Kabudi amewataka mawakili wa mashirika ya umma ambao wamekuwa wakisimamia kesi mbalimbali kutoa taarifa kwa Ofisi ya wakili mkuu wa serikali na siyo kusubiri hadi mambo yawe magumu.

Prof. Kabudi amebanisha hayo leo June 18,2021 jijini Dodoma wakati akifungua  mkutano mkuu wa watumishi wa Ofisi ya Wakali mkuu wa serikali ambapo amesema Mawakili wote wa Mashirika ya umma lazima wawajibike kwa Wakili Mkuu wa Serikali. 

“Mawakili wote wa mashirika ya umma lazima wawajibike kwa Wakili mkuu wa serikali na kesi zote lazima waripoti kwa Wakili mkuu siyo kusubiri hadi mambo yanakuwa magumu ndiyo wanaripoti”amesema.

Aidha,Waziri Kabudi amesema kuwa ipo haja ya kuimarishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali ili kusaidia kusimamia mashauri yote yanayoikabili serikali ya ndani na nje ya nchi.

Prof. Kabundi amesema kuwa hali hiyo itasaidia kuiondolea mzingo Serikali  wa gharama kubwa ya fedha  ambayo imekuwa ikitumia kwa ajili ya kulipa mawakili wa nje ya nchi.

 Pia amesema kuwa ipo haja ya kuwa na taasisi ya mafunzo ya mawakili wa Ofisi ya serikali ambayo itatumika kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kuimarisha utendaji kazi wao.

Amesema hali hiyo itasaidia taifa kuondokana na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kulipa mawakaili wa nje pale taifa linapofunguliwa kesi nje ya nchi.

“Hawa viongozi wetu Mama Samia hata wakati ule wa Hayati Magufuli wanapata shida sana unakuta wametenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye miundombinu au miradi ya maendele lakini unakuta nchi inashitakiwa na kwenda mahakani unatakiwa kutumia fedha nyingi sana kulipa mawakili”amesema Prof. Kabudi

Pia, amesema kuwa kesi ambazo zimekuwa zikifunguliwa zinailazimu nchi kulipa mamilioni ya fedha ambayo yangetumika katika miradi mingine ya maendeleo.

“Hivi sasa tuendelea tu na hiki kipindi cha mpito lakini baadaye nataka ofisi hii ndiyo iwe inasimamia kesi zote za serikali za ndani na nje tutafanikiwa tuu kama tutaendelea kuimarisha Ofisi hii ya Wakali mkuu wa serikali,”amesema

Kwa upande wake ,Wakili Mkuu wa serikali, Gabriel Malata,ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa madai dhidi ya Serikali kuhusu Gesi na Madini katika kuelekea uchumi wa Viwanda kutokana na wanasheria wengi kutokuwa na uelewa wa masuala hayo.

Amesema wanakabiliwa na   changamoto ya ukosefu wa watumishi 312  ambapo amedai waliopo ni  143 hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia ili kazi ziweze kufanyika kiweledi.