Home Mchanganyiko STOF RUVUMA ILIVYOSAIDIA VIJANA KUFUNGUA KAMPUNI ZAO NA KUAJIRI WENGINE

STOF RUVUMA ILIVYOSAIDIA VIJANA KUFUNGUA KAMPUNI ZAO NA KUAJIRI WENGINE

0

kijana Viviana Komba ambaye amefanikiwa kuanzisha kampuni ya kutengeneza nepi za watoto  kwa kutumia pamba laini

vijana waliopata mafunzo na mitaji kutoka Taasisi ya STOF  wakipata maelekezo ya kuboresha biashara zao  kutoka kwa Mkrugenzi wa STOF Teresa Nyirenda Msamala mjini Songea

Kijana Galus Mpepo  ambaye apewe mtaji wa kufungua kampuni ya kilimo na ufugaji katika eneo la Mlilayoyo wilayani Namtumbo.
****************************

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

TAASISI ya Saint Teresa Orphans Foundation(STOF) inayofanyakazi

mkoani Ruvuma nchini Tanzania na nchini Marekani kupitia mfumo wa

TEDNA imeweza kuwapatia vijana mafunzo ya ujasiriamali na kufanikiwa

kufungua kampuni zao.

Mkurugenzi wa STOF Teresa Nyirenda anasema Taasisi yake imeamua

kuanzisha mfumo wa TEDNA baada ya kubaini kuna kundi kubwa la vijana

wamemaliza vyuo vya kati na vyuo vikuu wamekosa ajira.

Nyirenda anasema kupitia TEDNA vijana waliomaliza vyuo vikuu

wameunganishwa na kupewa mafunzo na mitaji ili waweze kujiajiri na

kuajiri vijana wengine waliokosa ajira.

Vijana kadhaa mkoani Ruvuma kupitia Taasisi ya STOF wamepata

mafunzo na mitaji hivyo kufanikiwa kufungua kampuni zao chini ya

usimamizi wa TEDNA.

Galus Mpepo ni kijana wa Songea ambaye amelelewa na STOF tangu

akiwa na umri wa miaka nane ambapo hivi sasa ni mhitimu wa chuo kikuu

ambaye alipata changamoto ya ajira.

Mpepo anasema kutokana na changamoto hiyo STOF iliamua kuwapatia

mafunzo na kuwawesha kuanza biashara na kumiliki kampuni yenye

uwezo wa kuzalisha nyama za kusindika na kusindika bidhaa mbalimbali

kama unga na maharage.

Hata hivyo anasema amejikita zaidi katika kilimo ambacho kitamwezesha

kupata malighafi za mashambani kama mahindi,soya,alizeti ambazo

anazitumia katika ufungaji wa kuku na nguruwe.

“Hivi sasa natumia muda wangu zaidi katika kuimarisha kampuni yangu

ambapo nimeanzia kufanya shughuli za uzalishaji katika eneo la Mlilayoyo

wilayani Namtumbo,katika eneo langu kuna sehemu nimelima mashamba

na eneo linguine nimefuga mifugo kuku na nguruwe’’,anasema Mpepo.

Kwa upande wake Romana Haule mnufaika wa TEDNA anasema

amefanikiwa kuanzisha kampuni ya chakula ambapo hivi sasa

anawafanyakazi watatu.

Anaishukuru Taasisi ya STOF kwa kumwezesha mafunzo na mtaji hivyo

kufanikiwa kuanzisha biashara hiyo kupitia mfumo wa ujasiriamali wa

TEDNA ambapo hivi sasa ameweza kuwatunza watoto wake na kuwalipa

mshahara wafanyakazi wake.

Naye Zesco Ngonyani ni mmoja wa vijana waliofanikiwa kuanzisha

kampuni ya ujenzi kupitia mfumo wa TEDNA ambapo anasema STOF

imemsaidia kumpeleka shule hadi kumaliza kupata mafunzo ya ufundi

ujenzi ambapo awali alikuwa anafanyakazi mitaani bila usimamizi

madhubuti.

“STOF waliniangalia na kuona mafanikio yangu yanachelewa

ndipo,wakanisaidia kuanzisha kampuni ya ujenzi nikiwa na vijana

wenzangu,kwa hiyo hivi sasa Napata tenda za kujenga majengo kuanzia

msingi hadi kuezeka na umaliziaji wote ikiwemo kupaka rangi’’,anasema

Ngonyani

Anasema Kampuni yake ina mafundi bora,wenye uwezo wa hali ya juu na

kwamba wanafanya kazi kwa uaminifu mkubwa hali ambayo imesababisha

kampuni yao kuaminika na kupata kazi nyingi.

Anasema kampuni yake ina uwezo wa kufanya kazi zote zinazohusika na

ujenzi kuanzia kujenga,kuezeka,kupaka rangi,kuchomelea,kuweka

umeme,kutengeneza samani na kwamba mteja akikabidhi ramani ya

nyumba wao wanamaliza kila kitu na kumkabidhi nyumba iliyokamilika kwa

asilimia 100.

Anatoa shukurani kwa STOF kwa kumpeleka shule,kupata mafunzo na

kupewa mtaji hali ambayo inamwezesha kuanzisha kampuni ya ujenzi hali

ambayo imwezesha kuajiri vijana wengine.

Viviana Komba ni miongoni mwa vijana ambao wamesaidiwa na STOF

tangu akiwa na umri wa miaka nane ambapo amesomeshwa hadi elimu ya

chuo kikuu katika fani ya ualimu.

Viviana anasema baada ya kumaliza chuo kikuu alikosa ajira hivyo

Mkurugenzi wa STOF Teresa Nyirenda alivyoona vijana wengi wanamaliza

vyuo na kukosa ajira alianzisha TEDNA ili kuwakuza kifikra na kimtazamo

vijana na kuwapatia mitaji ili waweze kufanya biashara na kufungua

kampuni zao.

Anasema walipewa mafunzo mbalimbali kabla ya kupewa mitaji ambapo

yeye alipata wazo la kuanzisha kampuni ya kutengeneza nepi za watoto

kwa kutumia pamba laini ambazo hazina madhara kwa watoto

ukilinganisha na nepi za dukani.

Kupitia kampuni yake,Viviana anasema anatengeneza sabuni za maji,dawa

za kusafishia masinki,anatengeneza mablankenti ya watoto,mapambo ya

shingoni na mkononi,pochi za shanga na vikoi vya kimasai.

“Nina mashine za kisasa zinazoniwezesha kutengeneza bidhaa hizo,lengo

langu ni kumiliki kampuni kubwa itakayoajiri watu na kuwasaidia vijana

wengine ambao wapo mitaani hawana ajira’’,anasisitiza.

Hata hivyo anasema bidhaa ambazo amezitengeneza baadhi ameshaanza

kuuza na kwamba bado bidhaa nyingine zipo kwenye mchakato wa

kutengeneza jina la kibiashara ili hatimaye kuziingiza sokoni.