Home Mchanganyiko CHAVITA YAOMBA MTAALA MAALUM WA KUFUNDISHIA WANAFUNZI VIZIWI

CHAVITA YAOMBA MTAALA MAALUM WA KUFUNDISHIA WANAFUNZI VIZIWI

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Dickson Mveyange,akifungua Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Taifa (CHAVITA) Bw.Nidrosy Mlawa,akitoa mada mbalimbali wakati wa semina ya Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

Mratibu wa Mradi wa Kukuza hadhi ya Lugha ya alama ya Tanzania Bi.Lupi Maswanya,akielezea umhimu wa lugha katika mawasiliano wakati wa Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki Wazazi na Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa semina ya Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

Mwalimu Mary Masangula kutoka shule ya Msingi Kigwe -Viziwi,akizungumzia changamoto zinazowapata watu wenye uziwi katika maeneo yao ya kazi wakati wa semina ya Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

Mwalimu Brenda Mpina kutoka shule ya Msingi Chinangali akizungumzia wakati wa semina ya Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo yaliyofanyika leo Juni 8,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

CHAMA cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) kimeiomba Idara ya Elimu nchini  kuwa na mtaala maalum wa kufundishia wanafunzi viziwi mashuleni ili waweze kuendelea na Elimu ya juuu.

Hayo yamesemwa leo Juni 8,2021 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Dickson Mveyange,wakati wa Mafunzo na Kampeni Kuhusu Ukiziwi na Lugha ya Alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo.

Bw.Mveyange amesema kuwa ,mitaala inayotumika mashuleni ni ya jumla na haiwazingatii viziwi Pamoja na kuwa kuna tofauti ya wanaosikia na viziwi  hali ambayo ni kikwazo kwa watoto hao ambao wanatakiwa kupewa Elimu maalum badala ya Elimu ya jumla.

Amesema kuwa ,licha ya Idara ya maendeleo ya Jamii kuridhia kuwepo kwa lugha ya alama lakini inaonekana  bado halijatekelezwa ipasavyo na kusababisha wanafunzi wengi viziwi kushindwa kuendelea na masomo Kutokana na ugumu wa lugha ya Mawasiliano.

“Bado Kuna mapungufu mengi,tunahitaji maboresho zaidi ili kuweka usawa kwa jamii na viziwi nao waweze kusoma bila kubaguliwa,bado ukosefu wa misamiati ya masomo ya sayansi, uraia na historia ni changamoto,hivyo vinapaswa kuangaliwa upya,”amesisitiza

“Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Mtaala uliopo unawanyima wanafunzi  fursa ya kufikia malengo yao katika masomo”ameongeza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Taifa (CHAVITA) Bw.Nidrosy Mlawa,ameitaka jamii kuwashirikisha viziwi kwa mambo yote ili maendeleo yasimwache mtu.

Bw.Mlawa amesema kuwa ili kuifikia Tanzania ya ndoto za walio wengi lazima kuwepo marekebisho Katika mitaala ya Elimu ili watu wenye mahitaji maalum wasibaki nyuma.

“Kuna hili suala la  ufinyu wa muda katika vipindi, sehemu kubwa ya wanafunzi wenye uziwi hawawezi kumaliza maswali katika majaribio ya saa moja na nusu  kwani wao swali moja hutumia dakika tano ili waweze kupata jibu sahihi,”amefafanua.

Aidha amesema kuwa Mtaala wa elimu ni mwongozo wa masomo unaotoa dira ya mafunzo yanayotakiwa katika utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi katika ngazi fulani ya elimu

Naye Mwalimu Marry Masangula kutoka  shule ya msingi Kigwe-Viziwi Dodoma,ameeleza kuwa kwa sasa wanafunzi wenye uziwi hutumia muda mwingi hadi kumaliza elimu yao ya msingi kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu sahihi kuwawezesha kuelewa masomo.

“Ili waelewe vyema wanafunzi wenye uziwi kama sisi walimu tunapaswa kutumia zaidi lugha ya alama pamoja na vitendo kuwaelimisha lakini Jambo hili bado ni gumu kwa kuwa walimu pia hawatoshelezi,”amesema Mwalimu

Mwalimu Masangula amesema kwa kawaida ratiba iliyopo kwenye mtaala wa sasa inampa mwalimu dakika 40 tu za kufundisha ikiwa ni muda sawa kwa wanafunzi wote wa shule ya msingi wenye mahitaji maalum na wasio walemavu,Dakika ambazo zaelezwa kutotosha kuwafundisha watoto hao wenye mahitaji maalum.

“Kufundisha ni dakika zilezile 40 na mada ni ile ile sawa na wanafunzi wanaosikia vyema,hii ni changamoto kwa sababu inabidi umfundishe mwanafunzi mmoja mmoja, wakati hawa wanahitaji vitendo zaidi kuliko maneno,” amesema .