Home Mchanganyiko RC MTAKA AITAKA NACTE KUANDAA MKUTANO WA KUTATHIMINI MAONYESHO YA PILI ELIMU...

RC MTAKA AITAKA NACTE KUANDAA MKUTANO WA KUTATHIMINI MAONYESHO YA PILI ELIMU YA MAFUNZO NA UFUNDI

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa maelezo kwa wandaaji wa Maonyesho kabla ya kuanza kukagua mabanda  katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthoni Mavunde wakielekea kwenye mabanda ya taasisi mbalimbali  katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Kenneth Boimanda alipotembelea banda la TANESCO  katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo cha Takwimu na Mashariki mwa Afrika Bw.Eusebius Mwisongo mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.kushoto ni Afisa Udahili wa chuo hicho Samuel Marandu. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthoni Mavunde wakionja chai yenye mchanganyiko maalumu katika banda la wajasiriamali   katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akiweka saini katika kitabu cha wageni, alipotembelea banda la NACTE katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini,Josephat Maganga,akizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka  kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru,akizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka  kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto ,akizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka  kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga,akizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka  kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amelitaka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuandaa mkutano wa tathimini ya maonyesho ya vyuo vya ufundi ili kuona tija ya maonyesho hayo.

Kauli hiyo aliitoa jana mara baada ya kutembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea  katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mtaka amesema kuwa watafanya kikao cha kujadili namna pia ya kuwaendeleza wabunifu wa maonyesho hayo ili kazi zao ziwe na tija kiuchumi zaidi.

“Naomba NACTE baada ya maonyesho haya kuhitimishwa,muandae mkutano wa tathimini tukae pamoja na tujadili mambo mablimbali ya maonyesho haya zikiwemo changamoto ili tujue namna ya kuzitatua ili tukapoandaa maonyesho ya mwakani yawe na tija zaidi.”amesema Mtaka

Pia ameitaka NACTE kuhakikishe mwakani mkoa unakuwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano haya,ili kusaidia kutangaza maonyesho hayo kikamilifu na kutoa hamasa kwa wananchi kuja kutembelea mabanda na kununua bidhaa zinazouzwa. 

Mtaka amesema  kuwa lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kutaka kuboresha maonyesho hayo ya vyuo yaliyoandaliwa na NACTE ili yawe na msisimko zaidi kwa wananchi.

“Naamini kwamba maonyesho  yajayo yakiboreshwa yatabadili taswira na kuwa sehemu ya kuchevusha biashara ya mkoa ikiwemo kukuza teknolojia katika sekta mbalimbali kama Kilimo,ufugaji na vingine.” amesisitiza.

Pia Mhe.Mtaka amesema kuwa  wao kama Mkoa wako tayari kushirikiana na waandaaji wa maonyesho ikiwemo kuwa na sehemu ambayo italea na kukuza wabunifu ambao watakuwa wamebuni teknolojia mbalimbali kupitia kwenye maonyesho husika.

Aidha Mhe.Mtaka  amewaomba waandishi wa habari kuhakikisha wanashirikiana na NACTE au taasisi nyingine zote kuhakikisha wanayatangaza maonyesho hayo kwa siku zilizobaki ili jamii ijue na kujitokeza kutembelea katika viwanja hivyo.

Hata hivyo amezishauri Benki na Taasisi za fedha kutenga fedha kwa ajili ya kuwadhamini wabunifu nchini ili kuendeleza vipaji vyao.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt.Adolf Rutayuga amesema kuwa wao kama NACTE watayafanyia kazi ushauri na maoni yote aliyoyatoa ili kuleta tija zaidi katika maonyesho hayo mwakani.