Home Michezo LIVERPOOL YAICHAPA 4-2 MAN UNITED PALE PALE OLD TRAFFORS

LIVERPOOL YAICHAPA 4-2 MAN UNITED PALE PALE OLD TRAFFORS

0
Manchester United wamechapwa mabao 4-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 34, Roberto Firmino dakika ya 45 na 47 na Mohamed Salah dakika ya 90, wakati ya Man United yamefungwa Bruno Fernandes dakika ya 10 na Marcus Rashford dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 35 na kusogea nafasi ya tano, ikizidiwa pointi nne na Chelsea ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.
Man United yenyewe inabaki na pointi zake 70 za mechi 36 sasa katika nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa tayari, Manchester City wenye pointi 80 za mechi 35.