Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kupitia Rasimu ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambayo inatarajiwa kuwasilishwa hivi karibuni, Bungeni, jijini Dodoma. Wapili kulia ni Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo, Kushoto ni Katibu Mkuu, Christopher Kadio, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma, leo, na kuhudhuriwa na Watendaji Wakuu wa Wizara pamoja na Taasisi zake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akizungumza katika Kikao cha Kupitia Rasimu ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambayo inatarajiwa kuwasilishwa hivi karibuni, Bungeni, jijini Dodoma. Wapili kulia ni Katibu Mkuu, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, wakiangalia nyaraka za Rasimu ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara wakati wa Kikao cha Kupitia Rasimu hiyo kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kulia), akizungumza jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee, wakati wa Kikao cha Kupitia Rasimu ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara kilichoongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani), katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kupitia Rasimu ya Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 ya Wizara yake, katika kikao kilichohudhuriwa na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.