Home Mchanganyiko WAZIRI WA UCHUMI NA UWEKEZAJI AWAFUNDA VIONGOZI KUHUSUN UZALENDO NA USALAMA WA...

WAZIRI WA UCHUMI NA UWEKEZAJI AWAFUNDA VIONGOZI KUHUSUN UZALENDO NA USALAMA WA TAIFA KATIKA UWEKEZAJI

0

Mkurugenzi  Mtendaji wa CRDB Bank Abdulmajid Nsekela (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na  Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga Uzalendo na Usalama wa Taifa  katika Uwekezaji kwa Viongozi yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMA -JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele  (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kaz, Uchumi na  Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga uzalendo na  Usalama wa Taifa  katika Uwekezaji yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC

Mkuu wa Wilaya Pangani Zainab Abdalah  (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga Uzalendo na  Usalama wa Taifa  katika Uwekezaji kwa viongozi yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC.

****************************

Na Kapteni Selemani Semunyu-JWTZ 
Waziri Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mh Mudrik Soraga amewataka makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu wakiwemo wa Wilaya, Wakurugenzi kutoka Taasisi za Umma na Binafsi ikiweko wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama kuzingatia Usalama wa Nchi katika Majukumu yao.

Alisema hayo Mwishoni mwa Wiki wakati wa kufunga Mafunzo  Maalum kozi fupi (Capstone)kundi la Kumi 2021 inayotolewa  na Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi Nchini NDC kutoka Sekta binafsi na sekta za Umma yenye lengo la kuangazia Usalama wa Taifa katika Uwekezaji  iliyofanyika kwa siku tano Jijini  Dar es Salaam.

Alisema mafunzo hayo ni adhimu yenye lengo la kujenga Viongozi na wafanyabiashara katika uzalendo wenye kuzingatia usalama wa taifa letu katika sekta yenye kuingizia serikali mapato ya uwekezaji na kuipongeza NDC kwa mafunzo hayo na kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya katika kuwajenga viongozi.

“Mliopata mafunzo haya nataka mkawe chachu kwa wale amabao hawajayapata na kuwa tofauti katika Utendaji na Watendaji wengine ambao hawajapata mafunzo hayo kwani ni nafasi pekee amabayo sio kila kiongozi anaweza kuipata.” Alisema Waziri Solaga.

Awali Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Ibrahim Muhona alisema mchanganyiko wa kozi hiyo unatokana na ukweli kwamba sekta rasmi na sekta binafsi zinategemeana katika kukuza uchumi  hasa katika kipindi hiki cha kuingia uchumi wa kati wa juu kama ilivyo dira ya mwaka 2025.

“Hali ya usalama na amani katika nchi yetu ni muhimu sana kwa jamii ya Watanzania na maendeleo kwa ujumla hivyo nyinyi ni wadau muhimu katika kuhakikisha adhma hiyo inatimizwa kikamilifu. Alisema Brigedia Jenerali Mhona

Kwa upande wake mwakilishi wa Wahitimu hao na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
” Tulitamani muda Uonghezwe kwani mijadala iliyotokana na mada muhimu zilizowasilishwa zilikuwa muhimu mno ila wanamatumaini makubwa pia mapendekezo waliyoyatoa yatafanyiwa kazi.
Mafunzo hayo yaliwakutanisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa taasisi za umma na binafsi hususani wafanyabiashara kama wadau wa usalama wa Taifa  ambao wanawajibu wa kuhakikisha taifa letu linakuwa na amani  ustawi mzuri kwa ujumla.