Home Mchanganyiko WAFANYABIASHARA WAOMBWA KUWA NA HURUMA WANAOFUNGA MWEZI WA RAMADHAN

WAFANYABIASHARA WAOMBWA KUWA NA HURUMA WANAOFUNGA MWEZI WA RAMADHAN

0

……………………………………………………………………………………………

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaomba wafanyabiashara nawatoa huduma mbalimbali mkoani humo kutopandisha gharama za mazao na mahitaji mbalimbali katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwahurumia Waislamu wanaoendelea na mfungo wa Mwezi wa Ramadhan.

“Niwaombe sana wafanyabiashara na watoa huduma, hiki sio kipindi cha kujineemesha ni kipindi cha tafakari, ni kipindi cha kuwa Pamoja, kipindi cha kuhurumiana, kipindi cha sadaka, sio kipindi cha kuona kwamba sasa ni kipindi cha kupata mapato Zaidi, niwaombe msiongeze bei za vyakula, niwaombe msiongeze bei za huduma mbalimbali, mwaka jana mlinisikiliza, hali ilikuwa nzuri, ni matarajio yangu hata mwaka huu pia, bei za vyakula sokoni, viazi, mihogo, sukari na bidhaa nyingine hazitapanda,”

“lakini kama itatokea watu wataokwenda kinyume, niwatahadharishe, serikali ipo na itafuatilia kila mahali, ili tusitese watu ambao tayari wanajitesa, mtu anajinyima, anashinda njaa, anakula jioni ile na wewe unaamua kumtesa Zaidi, kuwabebesha mzigo mkubwa Zaidi, hii haikubaliki, tuhurumiane, tupendane, bila ya shaka ujumbe huu utafika kwa kila mwananchi na kila mwanarukwa,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo alitoa ujumbe huo tarehe 14.5.2021 ambapo Waislamu kote nchini walikuwa wameuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kipindi cha siku 30 ama 29 kutemea mwandamo wa mwezi.