Home Mchanganyiko TANZANIA ITENDELEA KUSHIRIKIANA NA INDIA KATIKA KUHAKIKISHA MAZINGIRA BORA YA KIBIASHARA KWA...

TANZANIA ITENDELEA KUSHIRIKIANA NA INDIA KATIKA KUHAKIKISHA MAZINGIRA BORA YA KIBIASHARA KWA WAFANYABIASHARA

0

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu fursa za biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India katika mkutano kwa njia ya mtandao kati ya nchi hizo uliofanyika 15/04/2021 Mtumba, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akiongea kuhusu kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara pamoja na fursa za uwekezaji kati ya  Tanzania na India katika mkutano kwa njia ya mtandao kati ya nchi hizo uliofanyika  15/04/2021 Mtumba, Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akiwa na  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) (Kushoto) wakiwa katika mkutano kwa njia ya mtandao kati ya  Tanzania na India uliofanyika  15/04/2021 Mtumba, Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) (Kushoto) wakiwa na Mkurugenzi Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara  Bw. Ali Gugu  (Katikati) na Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ombeni Mwasha wakiwa  katika mkutano kwa njia ya mtandao kati ya  Tanzania na India uliofanyika  15/04/2021 Mtumba, Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb)  akiwa pamoja na sehemu ya Watumishi ya Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara katika mkutano kwa njia ya mtandao kati ya  Tanzania na India uliofanyika  15/04/2021 Mtumba, Dodoma. 

………………………………………………………………………………

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo  amesema Tanzania itendelea kushirikiana na India katika kuhakikisha mazingira bora ya kibiashara kwa wafanyabiashara pamoja na kuendeleza za uhusiano wa kidplomasia kijamii na kiuchumi  katika nchi hizo.

Profesa Mkumbo ameyasema hayo alipokuwa akishiriki katika mkutano kibiashara  kwa njia ya mtandao  kati ya India na Tanzania Mkutano  uliofanyika tarehe 15/04.2021 katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Mkutano huo ulilenga kujadiliana kuhusu fursa za biashara zilizopo, kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kubadilishana uzoefu na kuonyesha   maeneo muhimu ya biashara kati ya India na Tanzania. 

Akiongea katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Balozi wa India nchini Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini India, pamoja na wenyeviti wa wafanyabiashara katika nchi hizo, Waziri aliwashauri wawekezaji kutoka India kuwa wakiwekeza Tanzania wataweza kuuza bidhaa na huduma zao katika nchi za Afrika Mashariki (EAC) na nchi za Jumuiya  ya Maendeleo kusini mwa Afrika(SADC) bila ushuru wa forodha na ukomo wa kiwango cha bidhaa kama ilivyo kwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Akiwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, Waziri alisema kuwa Tanzania ni mwananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye ukubwa wa soko lenye idadi ya watu wasiopungua milioni 177. Pia Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendelea Kusini mwa Afrika yenye  ukubwa wa soko lenye idadi ya watu  zaidi  milioni 300. Vilevile Tanzania iko katika hatua za mwisho za kukamilisha majadiliano ya uanzishaji wa Eneo huru la Biashara Afrika litakalokuwa na ukubwa wa soko lenye idadi ya watu isiyopungua bilioni 1.5.

“Hivyo, kwa kuzingatia jinsi India ilivyoendelea katika Sekta ya Viwanda na Biashara, nawahimiza wafanyabiashara wa India kuja hususani wenye Viwanda kuja kuwekeza katika maeneo ya fursa zilizopo Tanzania hasa katika uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo, ngozi na madini”.

Aidha, Prof Mkumbo alizisihi taasisi za Serikali Tanzania na India kufanyia kazi vikwazo  vya kibiashara hususan vikwazo visivyo vya kiushuru (non- tariff barriers) ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma  baina ya nchi hizo huku wakizingatia ushindani katika biashara. Pi aliainisha kuwa  kwa sasa Tanzania inatekeleza Mpango wa “Blue Print” unaolenga kuboresha mazingira  ya biashara ili kuvutia biashara na uwekezaji. 

“  Nafikiri hatutakubaliana kuwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania kama viungo, mbaazi za kijani, korosho  na ufuta  ambavyo vinahitajika zaidi India  lakini havina soko la kuaminiaka. 


Vilevile, Waziri alisema ili kutimiza azma hiyo ya kuendeleza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo, Serikali ya Tanzania na India imeanzisha Tume ya pamoja ya Biashara ( Joint Trade Commission (JTC)) inayokutana mara moja  ambapo mkutano wa JTC unatarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Tanzania.