Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akikabidhiwa rasmi nyaraka za kuendesha ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na sasa ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe katika Kikao cha makabidhiano leo katika ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James baada ya kumkabidhi nyaraka za kuendesha ofisi rasmi katika kikao cha makabidhiano leo katika ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akiongea na menejimenti ya Wizara pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na sasa ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe leo katika ofisi za
Wizara, Mtumba jijini Dodoma
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara na sasa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe akiongea na menejimenti ya Wizara katika kikao cha makabidhiano leo katika ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James amekabidhiwa ofisi rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Riziki Shemdoe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI leo katika ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Makatibu Wakuu hao waliahidi kuendelea kushirikiana katika kazi mbalimbali hasa katika kuboresha muundo wa Maafisa Biashara wa Halmashauri kwa kuanzisha wa Kitengo cha Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili kurahisisha utendaji kazi wa wizara hizo kukuza biashara na kuendeleza viwanda vikubwa na vidogo vidogo vilivyopo katika halmashauri hizo.
Akiwashukuru wafanyakazi wote wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kufanya naye kazi vizuri kwa ushirikiano na Amani, Katibu Mkuu TAMISENI alitoa angalizo kwa Wizara kuendelea kusimamia na upatikanaji wa Sukari, Mafuta ya Kula, Mfumuko wa bei wa vyakula hasa katika mfungo wa mwezi ramadhani, na masoko kwa ajili ya mazao ndani na nje ya nchi.