Home Michezo SAMATTA AIPELEKA FENERBAHCE NAFASI YA PILI LIGI KUU YA UTURUKI

SAMATTA AIPELEKA FENERBAHCE NAFASI YA PILI LIGI KUU YA UTURUKI

0

Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Ally Samatta,ameipeleke nafasi ya pili timu yake ya  
Fenerbahçe baada ya kufunga bao 1-0 dhidi ya Denizlispor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki Uwanja wa Ülker Fenerbahçe Şükrü Saracoğlu Spor Complex Jijini İstanbul.

Samatta aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 64 akifunga bao kwa kichwa akimalizia  pasi ya beki ,Caner Erkin. 
Kwa ushindi huo, Fenerbahçe inafikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Beşiktaş inayoongoza na mechi moja mkononi, wakati Denizlispor inayobaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 30 inaendelea kushika mkia.