Home Michezo TANZANIA YAFUZU AFCON KIBABE YAIONDOSHA BURUNDI

TANZANIA YAFUZU AFCON KIBABE YAIONDOSHA BURUNDI

0

……………………………………………………………………………………………..

Licha ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kufungwa mabao 6-4 na Burundi imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-9.

Mchezo wa kwanza Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 8-3 hivyo unawafanya wafuzu kwa idadi ya Mabao 12-9.

Tanzania ilianza kipindi cha kwanza kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka dakika  ya pili kupitia kwa Erick Manyama na dakika ya sita lililofungwa na Jarufu Juma.

Burundi ambao katika mchezo wa leo walibadilika na kucheza kwa ubora mkubwa tofauti na mchezo uliopita walisawazisha dakika ya 8 na 10 kupitia kwa  Giggs Ishimwe na Nahimana Eliya.

Hadi dakika 12 za kipindi cha kwanza zinamalizika timu hizo zilikuwa sare kwa mabao 2-2.

Dakika nyingine 12 za kipindi cha pili timu hizo zilionekana kuvumbiana huku kikao mmoja akilinda vizuri lango lake na mwisho kipindi hicho kikamalizika bila yoyote kupata bao.

Dakika 12 za mwisho za Burundi walirejea kwa nguvu zaidi  wakicheza kwa maelewano makubwa  na kuwapa wakati mgumu Tanzania ambao walionekana kuchoka.

Katika kipindi hicho cha mwisho Burundi walifunga mabao matatu ya haraka  kupitia Ruginimugabo Ibrahim kabla ya dakika tano za mwisho Tanzania kuamka na kufunga mawili  kupitia kwa Erick Manyama na Ibrahim Ibadi