Home Michezo MASHINDANO YA MASUMBWI KWA WANAWAKE YA MALKIA ULINGONI YAAHIRISHWA KUPISHA MAOMBOLEZO

MASHINDANO YA MASUMBWI KWA WANAWAKE YA MALKIA ULINGONI YAAHIRISHWA KUPISHA MAOMBOLEZO

0

*************************************

Pambano la  masumbwi kwa Wanawake Queen of the Ring ‘Malkia wa Ulingo limeahirishwa hadi hapo baadae kupisha kipindi cha Maombolezo.

Mratibu wa Habari wa wakala wa Michezo Nchini wa  Peaktime Joyce Mbogo alisema  wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha  aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17/03/ 2021.

“Kufuatia Msiba huu hatuna budi kuahirisha Pambano letu lililokuwa lifanyike Machi 27 Ubungo Plaza na tutapanga tarehe nyingine baadae, alisema Joyce.

Alisema Msiba ni Mzito na Rais Magufuli atakumbukwa na wadau wa ngumi  ukizingatia pia Mapinduzi makubwa aliyoyafanya ya kutengeneza Kamisheni Moja kusimamia Mchezo huo.

Aidha alimpongeza Rais Mpya Mama Samia Suluhu Hassan na kumtakia kila la kheri katika majukumu mapya na kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Kwa upande wa mabondia watakaoshiriki pambano hilo aliwataka katika kipindi hiki cha maombolezo pia wakitumie kufanya mazoezi kujiandaa.

ALIWATAJA MABONDIA WATAKAOWANIA MKANDA WA DUNIA SIKU HIYO KUWA NI HALIMA VUNJA BEI ATAKAYEPIGANA NA ZULFA MACHO KATIKA MCHEZO WA ROUNDI 10.

MABONDIA WENGINE NI FATUMA YAZIDU  ATAKAYEPIGANA NA DOROTHEA MUHOZA, HAPPY DAUDI DHIDI YA LEILA YAZIDU NA LULU KAYAGE DHIDI YA JESCA MFINANGA.

WENGINE NI MWAMNE HAJI  DHIDI YA SARAFINA JULIUS,AGNES KAYANGE DHIDI YA MWAJUMA PENGO,GRACE MWKAMELE DHIDI YA ASHA GOTA WAKATI  SALMA KIHOMBWA DHIDI YA MARIAM MUNGI NA ZAWADI KUTAKA  DHIDI YA MARTHA KIMARO.