Home Michezo SIMBA SC YAZIDI KUTEMBEZA VICHAPO VPL, YAICHAPA JKT TANZANIA 3-0

SIMBA SC YAZIDI KUTEMBEZA VICHAPO VPL, YAICHAPA JKT TANZANIA 3-0

0

**************************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Simba Sc imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibamiza JKT Tanzania mabao 3-0 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba ilianza kupata bao la mapema likifungwa na Chris Mugalu dakika 8 ya mchezo na baadae Luis Miquissone kupachika bao la pili.

Kipindicha pili Simba bado ilionekana kutaka kuongeza bao baada ya kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la timu ya JKT Tanzania na baadae dakika 93 John Bocco kufunga ukurasa wa mabao kwa bao la tatu na la ushindi kwa klabu ya Simba.