Home Mchanganyiko RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MAKAMU WA...

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NYALI MTAMBWE PEMBA

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwao kuifariji familia kabla ya kufanyika kwa mazishi katika Kijiji cha Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba .

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume (kushoto kwa Rais) wakati alipofika nyumbani kwa marehemu kutowa mkono wa pole kwa familia, kabla ya kuaza kwa mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba) CDR.Mohammed Mussa Seif na Katibu wa Rais Dkt. Abdalla Hasnu Makame

WANANCHI wa Pemba wakihudhuria maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba

Maofisa wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa katika viwanja vya eneo la kaburi kwa ajili ya mazishi hayo yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa maziko yake yalifanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Maalim Seif Sharif Hamad, mazishi yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.

RAIS wa Zanzibar Mstaaf Awamu wa Sita Alhajj Dk. Amani Karume akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.(Picha na Ikulu)