Home Michezo YANGA SC YAMTANGAZA NIZAR KHALFAN KUWA KOCHA MPYA MSAIDIZI WA KAZE

YANGA SC YAMTANGAZA NIZAR KHALFAN KUWA KOCHA MPYA MSAIDIZI WA KAZE

0
KLABU Yanga SC imemtangaza rasmi mchezaji wake wa zamani na kocha wa African Lyon, Nizar Khalfan kuwa kocha mpya Msaidizi wa Mrundi, Cedric Kaze akichujua nafasi ya Juma Mwambusi aliyejiuzulu hivi karibuni kwa sababu za kiafya.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli, Nizar amepata nafasi hiyo baada ya kupita kwenye usaili uliofanyika Ijumaa ya Januari 22, mwaka huu.
Bumbuli amebainisha kuwa kulikuwa na makocha takribani 10 waliojitokeza kuisaka nafasi hiyo na watano walifikia hatua ya mwisho(fainali) akiwemo Salvatory Edward, Maalim Saleh na Omary Kapilima.