Home Michezo KMC FC YAACHANA NA WACHEZAJI WAKE WAWILI

KMC FC YAACHANA NA WACHEZAJI WAKE WAWILI

0

*********************************************

Wakati kipindi cha usajili wa dirisha dogo ukiendelea, KMC FC imeachana na wachezaji wake wawili ambao ni David Mwasa ambaye ameuzwa kwenda Mbeya City pamoja na Salim Aiyee kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba wake.

Salimu alijiunga na KMC kwa mkataba wa miaka mwili akitokea Mwadui FC ambapo ameitumikia Timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2021.

Kwa upande wa Mwasa ambaye alijiunga na KMC FC kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli, na hivyo kutumikia KMC FC kwa kipindi cha miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2022.

KMC FC inawashukuru wachezaji hao kwa mchango mkubwa walioutoa na tunawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.