Home Mchanganyiko SERIKALI KUBORESHA BWAWA LA MAJI HOROHORO

SERIKALI KUBORESHA BWAWA LA MAJI HOROHORO

0

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga
akizungumza wakati wa ziara yake katika miradi ya maji wilaya za Tanga,
Mkinga na
Muheza mkoani Tanga kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan
Kitandula na kulia aliyevaa kilemba ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga
Mhandisi Upendo Lugongo

Mbunge
wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula kushoto akizungumza wakati wa
ziara hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony
Sanga na kulia ni Diwani Mteule wa kata ya Horohoro(CCM) Merieyer Miliya

Meneja
wa Ruwasa wilaya ya Mkinga Mzee Kaijage akizungumza wakati wa ziara
hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula na kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akimsaidia
kufunga madumu kwenye baiskeli mmoja wa watoto aliowakuta wakichota maji
kwenye bwawa la maji horohoro wakati wa ziara yake  kushoto ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)
Mhandisi Geofrey Hilly na kulia ni Meneja Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi
Rashid Shabani

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akimsikiliza kwa
umakini Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dastan Kitandula wakati wa ziara
yake kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Maji Horohoro kutoka Tanga Uwasa
Mhandisi Salum Hamisi

Msimamizi
wa Mradi wa Maji Horohoro kutoka Tanga Uwasa Mhandisi Salum Hamisi
kushoto akisistiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi
Anthony Sanga wakati wa ziara yake

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akisalimia na
Diwani Mteule wa Kata ya Horohoro (CCM) Merieyer Miliya katikati ni
Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula na kushoto ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)
Mhandisi Geofrey Hilly

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akiingia kwenye
mradi wa Maji Horohoro wakati wa ziara yake ya siku moja kulia ni Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo na katikati ni Mbunge
wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa
Mhandisi Geofrey Hilly

Muonekano wa Bwawa ambalo ndio chanzo cha Maji kama linavyoonekana.  

 

SERIKALI imesema uboreshaji wa bwawa la maji la Horohoro
ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kinachotegemewa na wakazi wa mji huo
uliopo mpakani mwa Tanzania na Kenya utaanza muda mfupi na utakamilika
kwa wakati ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na
salama.
 
Hayo
yalisemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga
wakati wa ziara yake katika miradi ya maji wilaya za Tanga, Mkinga na
Muheza mkoani Tanga ambapo baada ya kutembelea eneo la bwawa hilo na
kupata taarifa kwamba huduma ya maji sio ya kuridhisha na ndipo alipotoa
kauli hiyo.
 
Alisema
bwawa hilo ambalo lilichimbwa na kupitia mradi wa TASAF na limekuwa  na
maji ambayo kimsingi yanakuwa yakipotea licha ya kujengwa miundombinu
mizuri ya kutibu maji na kusafirisha maji ikiwemo vituo vya kuchotea
maji lakini bwawa  halina maji.
 
“Kimsingi
nilipopata taarifa hizi zilinishutsha sana na nimekwisha kuwaambia
wataalamu kutoka wizarani wafike eneo hilo na hivi sasa wapo njiani na
nimewaambia wasiondoke hapo mpaka wampe ripoti ili ndani ya wiki mbili
waweze kufanya maamuzi ya dharura ili wananchi hao waweze kuondokana na
adha ya shida ya maji”Alisema
 
“Hatuwezi
kuona wananchi wanapata shida ya maji tukatulia wakati serikali ipo na
ina fedha za kujenga hiyo miradi na isitoshe tulikwisha kuwekeza na
kujenga vituo vya kutibu maji na kusukuma sasa bwawa haliwezi
kutushinda”Alisema Katibu huyo.
 
Kwa
kweli inatia huruma ukiona wanajenga nyumba na nzuri mji unakuwa ila
hawana maji na hapa  ni mpakani na maaeneo mengine mpakani unaweza
kushangaa watu wanakosa maji wakaenda hata kutafuta nchi jirani hivyo
hatutaki hilo litokee tunataka watu wa hapa wapate maji hapa hapa kwa
sababu vyanzo vipi na serikali ya awamu ya tano imejipanga vizuri
kuwahudumia wananchi hasa wanyonge “Alisema
 
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM)
Dastani  Kitandula  alimueleza katibu huyo kwamba bwawa hilo ndilo ambalo
linalotegemewa kwa ajili ya kunusuru maisha ya wananchi wa vijiji vya
horohoro ambapo changamoto ni kubwa ya maji
 
 Alisema kwamba wanashukuru
Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundmbinu ya kusambaza maji
lakini changamoto bado ni kubwa kwenye chanzo kuhakikisha wanazuia
upotevu wa maji unaotokana na bwawa hilo kuvuja na kulipanua bwawa na
kujenga tuta kubwa zaidi ili kuhakikisha wanavuna maji mengi lakini pia
kuwa na uhakika maji hayatapotea.
 
Mbunge
huyo alisema kwamba wanachokiomba kwa serikali wanajua zipo jitihada
wanazofanya lakini wanaomba walichukulia jambo hilo kwa ukubwa kazi
iliyofanyika ya tathmini tokea mwezi Mei mwaka huu wanaiomba yapewe
kipaumbele ili kunusuru hali hiyo hata timu iliyopo njiani ikifika
isiondoke mpaka ikamilisha kazi hiyo
 
“Kama
ulivyokuja tumefarijika kwa kuona umekuja na tunaamini baada ya ziara
yako hii mambo yatakuwa mazuri ili wananchi wa eneo hilo waweze
kuondokana na hii changamoto ambayo  ya maji inayowakabili”Alisema
Mbunge Kitandula.
 
Awali
akizungumza Diwani Mteule wa Kata ya Horohoro (CCM) Merieyer Miliya
alisema hali ya maji bado ni tatizo kutokana na kwamba maji yaliyopo
kwenye chanzo ni machache na hayatoshelezi kutokana na kwamba tuta
lililopo kwenye bwawa lilipasuka na kusabaisha maji kumwagika.
 
Alisema
tatizo la maji bado ni kubwa kutokana na wananchi wengi walikuwa
wakitegemea bwawa hilo na hata nchi jirani ya kenya wanategemea maji
kutoka hapo kwao hivyo waliomba lipanuliwe lakini wanaamini kwa ujio
wake kazi zitaanza.