Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania kesho jijini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge wakati akitoa taarifa Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania.

………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

MAANDALIZI ya uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa ajili ya sherehe  za kuapishwa kwa Rais Mteule John Magufuli yamekamilika kwa huku wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria kwa Mkoa wa Dodoma

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi yalivyokamilika  kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania.

Dkt.Mahenge amesema kuwa mpaka sasa kwa taarifa alizonazo ni kwamba  viongozi wa nje ya nchi wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Rais wa Uganda,Waziri wa Mkuu wa Mozambique,Rais wa Comoro huku  wengine wanaendelea kuthibitisha kushiriki.
Aidha Dkt.amesema kuwa mbali na viongozi wa Kimataifa watahudhuria wakiwemo viongozi wakuu wastaafu.
Dkt.Mahenge amesema kuwa maandalizi yote ya uwanja yapo vizuri  ambapo vifaa vyote vinavyotakiwa vimefungwa ,sehemu ya kuapishiwa imewekwa vizuri.
“Pia maeneo ya nje kwenye uwanja wa barafu pameandaliwa vizuri kwa ajili ya watu kukaa na viti zaidi ya 10,000 vinewekwa na screen zitawekwa katika eneo hilo ili kuwawezesha wananchi  kuona kila kinachoendelea ndani ya uwanja.

Aidha amesema kuwa maandalizi ya sherehe hizo yamefanyika kwa kutumia fedha za ndani jambo ambalo ni matokea ya Rais ya kukusanya kodi.

Dkt. Mahenge amesema kuwa Rais Magufuli ataapishwa jijini Dodoma ambapo itawekwa historia ambapo kwa mara ya kwanza rais kuapishwa nje ya jiji la Dar es salaam.

“Tukiwa tunaingia katika historia tangu kupata uhuru kwa mara ya kwanza sherehe hizi zitafanyika Dodoma na siyo Dar es salaam kama ilivyo zoeleka”amesema

Dkt.Mahenge ametumia fursa hiyo kuwataka wanadodoma na wananchi wote kwa ujumla kutoka mikoa mbalimbali kuhudhuria kwa winginkatika shughuli hiyo