Home Mchanganyiko TAMKO LA VIONGOZI WA DINI MKOA WA TABORA

TAMKO LA VIONGOZI WA DINI MKOA WA TABORA

0

Askofu wa Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tabora Dkt. Isaac Kissiri Laiser akitoa mchango wake jana katika kikao cha Kamati ya Amani Mkoa wa Tabora kuhusu uchaguzi ujao.

……………………………………………………

Kutokanana na michango yetu wote tuliyoitoa sisi viongozi wa dini mkoa wa Tabora tunatoa matamko yafuatayo:-

 

1.      Watanzania  wote tuthamini Utanzania wetu kabla ya jambo lingine, tukizingatia kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

 

2.      Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tabora kwa pamoja tunasema Amani ni muhimu sana katika nchi yetu, hivyo tudumishe Amani wakati huu wa kuelekea uchaguzi, tuache mihemko ya kisiasa.

 

3.      Tunapenda kuwaasa wazazi wote, tuwaeleze watoto wetu/vijana wetu wasishawishiwe kuandamana au kuvuruga Amani ya Nchi yetu.

 

4.      Amani inapovunjika wahanga ni ndugu zetu, watoto wetu, dada zetu, wazee wetu na wote wasiojiweza

 

5.      Amani ikitoweka hakuna jambo litakaloendelea kama vile shughuli za kiuchumi, kilimo, biashara na shughuli mbalimbali hata za kidini.

 

6.      Amani ikitoweka inapelekea uharibifu wa miundombinu kama vile barabara, reli n.k.

 

7.      Upigaji kura haufanywi kwa misingi ya kidini, ukabila, rangi, ukanda, maumbile ya mtu au hali yake.  Hivyo mwananchi yeyote anaweza kumchagua kiongozi yeyote bila kujali yaliyotajwa hapo juu.

 

8.      Katika zoezi zima la uchaguzi tunawasihi mamlaka husika tuzingatie haki, wajibu na uadilifu kwa wadau wote.

 

9.      Wagombea wote na Wapiga kura wawe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi hata kama ni kinyume na matarajio yao na wasiporidhika wafuate taratibu za kisheria zilizowekwa.

 

10.   Viongozi wa dini tusitumie mimbali zetu  za mahubili kushabikia chama chochote.

 

11.   Viongozi wa dini Mkoa wa Tabora tunawaomba waumini wa dini zote tujitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya tarehe 28 Oktoba, 2020 na baada ya kupiga kura turudi majumbani kwetu ili tusubiri matokeo.