Home Michezo AZAM FC HAIKAMATIKI LIGI KUU VODACOM YAICHAPA 3-0 MWADUI FC

AZAM FC HAIKAMATIKI LIGI KUU VODACOM YAICHAPA 3-0 MWADUI FC

0

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 3-0 usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji wake Obrey Chirwa dakika za 28 na 63 pamoja na Prince Dube dk 61.

Kwa ushindi huo , Azam FC inafikisha pointi 18 baada ya kucheza sita na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba na mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao hata hivyo wamecheza tano.
Ushindi wa Azam FC leo hii umetokana na mabao ya washambuliaji wake wa kigeni, Mzambia Obrey Chirwa aliyefunga mawili dakika za 28 na 63 na Mzimbabwe, Prince Dube dakika ya 61.