Home Mchanganyiko RC- NDIKILO APIGA MARUFUKU UUZAJI WA KOROSHO PWANI KWA KUTUMIA MFUMO WA...

RC- NDIKILO APIGA MARUFUKU UUZAJI WA KOROSHO PWANI KWA KUTUMIA MFUMO WA KANG’OMBA

0

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano na wadau wa zao la korosho kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa huo kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali kuhusiana na msimu mpya wa uuzaji wa korosho pamoja na kuzungumzia changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi. Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dolphine Magere akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na wakulima  kuhusiana na mikakati  na mipango ambayo imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa zao la korosho ili kuweza kujiandaa na msimu mpya wa zao hilo. Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma akielezea jambo kuhusiana na jinsi alivyojipanga kikamilifu katika kuwasaidia wakulima wa zao la korosho kwa kusaidiana na maafisa wa kilimo pamoja na mabwana shamba ili kuwawezesha watimize malengo yao katika msimu mpya wa korosho.Baadhi ya wadau mbali mbali wa zao la korosho kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani ambao walihudhulia mkutano huo kwa ajili ya kujadili namna ya kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea katika msimu mpya wa zao ili pamoja na kuweza namna ya kutatua changamoto zinazowakabili katika zao la korosho.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

***********************************

NA VICTOR MASANGU, MKURANGA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amepiga amekemea na kupiga marufuku kwa baadhi ya wakulima kuuza zao la korosho kwa kutumia  mfumo  ambao haukubaliki unaojulikana kama  kang’omba na badala yake wahakikishe wanazingatia mwongozo uliwekwa na serikali wa kuuza korosho hizo kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuepukana na changamoto za kuwanyonya na kuwadhulumu haki zao  wakulima.

Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa mkutano na wadau mbali mbali wa zao la korosho pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kwa ajili ya kuweza kujadili namna ya kuweka mikakati ambayo itaweza kuwasaidia wakulima kuuza korosho zao katika msimu unaokuja  ikiwemo kuzitatua changamoto zinazowakabili.

“Sisis kama serikali ya Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawasaidia wakulima wetu wa zao la korosho kwa kuweka mipango mizuri na mikakati ambayo itaweza kusaidia kabisa kuondokanana nah ii hali ya kuwanyonya wakulima kwa kutumia mfumo wa kangomba hii haikubaliki hata kidogo kikubwa hapa inabidi vyama vya msingi viweze kulisimamia ili kwa kutumia mfumo halali wa stakabadhi ghalani”alisema Ndkilo.

Pia Ndikilo alisema kwamba katika kutimiza malengo amabyo wamejiwekea ni lazima wakulima wote wa zao la kurosho kuhakikisha kwamba wanazingatia taratibu zote za kilimo kwa kufanya usafi wa mashamba yao na kutoka uchafu wote ili korosho zisiweze kuharibika na hatimaye kuweza kupata korosho nzuri yenye ubora ambao unaweza kuwafanya wapate wanunuzi wengi.

Kadhalika aliongeza kuwa kilimo  cha zao la korosho ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kutokana na asilimia zaidi ya 80 wanategemea zao hilo katika kujiingizia kipato chao na kuondokana na wimbi la umasikini hivyo ndio maana serikali imeamua kulitilia mkazo suala hilo ili kuonyesha kwamba linaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kukuza uchumi wan chi.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa waliwaasa viongozi wa vyama vya msingi vya ushiriki kuwepo mipango madhubuti ya kuwatengenezea mazingira ambayo ni sahii wakulima wa zao la korosho katika kuelekea msimu mpya wa uuzaji ili waondokana na changamoto ya upatikanaji wa kupata soko kwa urahisi sambamba na kuzihifadhi katika maghala ambayo yametengwa maalumu.

Nao baadhi ya wakulima wa zao la korosho ambao wamehudhulia katika mkutano huo wa wadau hawakusita kutoa kilio chao kwa Mkuu wa Mkoa kuhusiana na changamoto inayowakabili ya ukosefu wa vifaa  maalumu kwa ajili ya kupimia ubora wa zao hilo pamoja na kuimba serikali iweze kuwasaidia kwa hali na mali upatikanaji wa pembejeo za kilimo pamoja na magunia.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Dolpine Magere amebainisha kwamba katika msimu ulipita kulikuwepo n achangamoto mbali mbali ambazo ziliweza kujitokeza ikiwemo kuwepo kwa mvua kubwa ambazo zilipelekea baadhi ya korosho kuharibika hivyo kwa sasa wamejipanga katika kujiandaa na msimu mwingine ambao unakuja.

Alisema zao la kurosho katika mkoa wa Pwani linachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato na kukuza uchumi kwa wananchi hivyo ni vema litakitiliwa mkazo  mkubwa ili wakulima waweze kunufaika kupitia zao hilo ambapo aliwahimiza waweze kuzingatia taratibu zote wanazopatiwa na wataalamu ili korosho zao ziweze kuwa na ubora mzuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma  amesema kwamba ili kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima ni lazima kuwashirikisha mabwama shamba katika kila hatua mbao wataweza kutoe elimu zaidi juu ya upandaji, ulimani  pamoja na utunzaji wa zao hilo kwa kuzingatia misingi ya taratibu zote zilizowekwa lengo ikiwa kupata ubora unaotakiwa.

Kilimo cha zao la korosho katika Mkoa wa Pwani kimekuwa ni moja ya mkombozi mkubwa katika kuwakomboa wananchi kuweza kuondokana na wimbi la umasikini na kuongeza pato la Taifa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini ili kuweza kuondokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima hao.