Home Mchanganyiko MRADI WA MAJI WA KYAKA –BUNAZI KAZI INAENDELEA

MRADI WA MAJI WA KYAKA –BUNAZI KAZI INAENDELEA

0

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji  Mhandisi Nadhifa Kemikimba akikagua eneo la ujenzi wa tanki katika mradi wa maji wa Kyaka – Bunazi. Kwa mbali kinachoonekana ni mto Kagera ambao ndicho chanzo cha maji cha mradi.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akitoa maelekezo kwa wataalam na mkandarasi, wakati akikagua eneo la ujenzi wa mfumo wa kutibu maji katika mradi wa maji wa Kyaka – Bunazi.

Mafundi wakiendelea na kazi katika eneo litakapo jengwa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni mbili za maji. Kazi inayofanyika hivi sasa ni uchimbaji na matayarisho ya kuweka msingi wa tanki.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akikagua michoro ya usanifu wa bomba, litakalotoka katika chanzo cha mto Kagera hadi katika mfumo wa kutibu maji. Mradi wa Kyaka – Bunazi unatekelezwa kwa fedha ya serikali na eneo mkandarasi analojenga  thamani yake ni bilioni 15 na kazi ya ulazaji mabomba itafanywa na wataalam  wa ndani wa Wizara ya Maji, kazi zote zinafanyika sanjari ili kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi haraka.