***************************************
Katika kuelekea siku ya msichana Duniani, Jamii na Wazazi nchini wamekumbushwa kuendelea kumlinda mtoto wa kike na vitendo vinavyomkandamiza ikiwemo kuzilinda haki zake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salama na Mshauri wa huduma ya simu kwa mtoto kutoka Shirika lisilo la kiserikali linaloangalia ulinzi wa mtoto (C-SEMA),Maria John , wakati akizungumzia Ofisini kwake ambapo amesema Kuwa Mtoto wa kike amekuwa akikumbana na Changamoto mbalimbali zikiwemo za miundombinu,Mimba za utoto, Umasikini,Mila potofu,ukeketaji,ndoa za utotoni na ukosefu wa taulo za kike Hali inayosabisha kurudishwa nyuma maendeleo yake.
Aidha ameiomba serikali kugawa Vifaa maalumu kwa watoto wa kike mashuleni pia elimu ya afya ya uzazi iwepo ya kutosha katika ngazi zote pia kukomesha tamaduni ambazo hazifai hususani zinazomkandamiza mtoto wa kike.
Kwa upande wao baadhi ya wasichana tuliozungumza nao, wamekili kukutana na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na kutokupewa kipaumbele na heshima katika jamii.
Nao baadhi ya wanaume wakizungumzia juu ya kuwafanyia vitendo hivyo vya kikatili Wasichna wamsema kuwa vimekuwepo huku wakiwataka baadhi ya wasichana kubadilisha mitindo yao ya maisha ikiwemo uvaaji mzuri wa mavazi yenye heshima ili kuepuka baadhi ya usumbufu.
Akizungumzia juu ya siku ya mtoto wa kike huu afisaTakikwimu na mawasiliano kutoka C-SEMA Itanisa Mbise, amesema Kuwa kwa mwaka huu wanatarajia kufanyia Mkoani shinyanga ambapo itaambatana na mashindano mbalimbali ya watoto wa kike na washindi 10 watapata zawadi.
Kauli mbiu ya siku ya msichana Duniani kwa mwaka ni tumuwezeshe mtoto wa kike ili kupata taifa sawa