Home Mchanganyiko WATOTO WA KIKE WATAKIWA KUTOA TAARIFA ENDAPO AKIFANYIWA UKATILI WA KIJINSIA

WATOTO WA KIKE WATAKIWA KUTOA TAARIFA ENDAPO AKIFANYIWA UKATILI WA KIJINSIA

0

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Baraka Makona akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC), Bi.Anna Henga akizungumza kwenye hafla ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakifanya maandamo ya amani kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam

Wakurugenzi mbalimbali wakipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule za msingi na Sekondari kwenye hafla ya maadhimisho ya Mtoto wa Kike Duniani yaliyofanyika kwenye leo Kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, watoto wa kike wametakiwa kutambua haki zao za msingi hivyo kutoa taarifa endapo ukiukwaji wa haki zao unapovunjwa hasa ukatili dhidi yao.

Ameyasema hayo leo Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Baraka Makona katika hafla ya kusheherekea Siku ya mtoto wa Kike Duniani ambayo imefanyika kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na Foundation mbalimbali zinazomlinda mtoto wa Kike Bw.Makona amesema kuwa wao kama serikali kushirikiana na wadau mbalimbali wapo kwaajili ya kuhakikisha haki kwa mtoto wa kike inalindwa.

“Matukio ya ukiukwaji wa haki unapotokea toeni taarifa mahali ambapo ni sahihi, kwa wakati katika sehemu ambazo zinahusika”. Amesema Bw.Makona.

Aidha amewataka watoto wa kike kuwa na nidhamu kwa walezi wao ili kuweza kutimizia ndoto zao na kuondokana na hali ya ukatili dhidi yao hasa kwa kukosa haki za msingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC), Bi.Anna Henga amesema kuwa mtoto anahaki ya ziada kama kulindwa na walezi pamoja na jamii inayomzunguka, mtoto wa kike pia ana haki za ziada tofauti na wengine hivyo.

“Tumesema tukaribishe hii siku kutoa uelewa kuhusu haki kwa mtoto wa kike kwamba anahaki za ziada ambazo zinatakiwa zitekelezwe”. Amesema Bi.Anna Henga.
 

Nao baadhi ya wasichana tuliozungumza nao, wamekili kukutana na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na kutokupewa kipaumbele na heshima katika jamii.

Vilevile kwa upande wa wavulana wao wamesema kuwa endapo wasichana hasa watoto wa kike wakifunzwa na kulelewa vizuri na walezi wao itawafanya wajiheshimu na kupunguza hali ya unyanyasaji kujitokeza kwa maana wengi wao hufanyiwa ukatili kutokana na ufinyu wa uelewa.