Home Michezo RIDHIWANI KIKWETE AIMWAGIA SIFA JEZI YA MSIMU MPYA KLABU YA AZAM FC

RIDHIWANI KIKWETE AIMWAGIA SIFA JEZI YA MSIMU MPYA KLABU YA AZAM FC

0
Mbunge Jimbo la Chalinze aliyepita bila kupingwa, Ridhiwani Kikwete akipokea jezi ya msimu mpya Klabu ya Azam FC kutoka kwa Meneja mauzo na masoko wa Klabu hiyo, Tunga Ally walipomtembelea Jimboni Chalinze.

………………………………………………………..

NA ANDREW CHALE
MBUNGE Jimbo la Chalinze aliyepita bila kupingwa, Ridhiwani Kikwete amezimwagia sifa jezi za msimu mpya za klabu ya Azam.
Ridhiwani Kikwete amesema jezi hizo zimetengenezwa kwa matirio bora na ya kisasa huku pia zikiwa katika muonekano mzuri na wa kuvutia kwa mvaaji.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa jezi hizo kama mdau wa michezo nchini, Ridhiwani Kikwete pia alipongeza mbunifu wa jezi hizo.
“Jezi hizi nzuri sana. Lakini pia utengenezaji wake mbunifu ametumia ubunifu wa hali ya juu hata  kwa kitambaa chake kuwa na uwezo wa kupenyesha jasho nje kirahisi anapokuwa anacheza uwanjani.” Alisema Ridhiwani Kikwete.
Kwa upande wake Meneja mauzo na masoko wa Klabu hiyo ya Azam fc, Tunga Ally,  walimpongeza Ridhiwani Kikwete katika kuthamini mchango wake katika michezo hivyo wameamua kumkabdhi jezi hizo kama mdau.
“Leo tumetembelea na kumkabizi jezi ya klabu ya Azam FC Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwa kutambua mchango wake mzuri  katika michezo Tanzania.” Alisema Tunga Ally.
Jezi hizo alizokabidhiwa Ridhiwani Kikwete ni pamoja na jezi Nyeupe ambayo itakuwa ya nyumbani, Bluu itakuwa ya ugenini huku ya Orange ikiwa ya ziada (neutral).
Aidha, jezi hizo mpya zimezinduliwa mwezi Agosti mwaka huu na tayari zinapatikana sokoni kwa bei poa kabisa ya Sh. 20,000 ikiwemo kwenye duka la klabu la Kariakoo ‘Azam FC Sports Shop’ na uwanjani Azam Complex. 
Azam FC ilianzishwa Julai 23, 2004 ikijulikana kama Mzizima SC na  kusajiliwa Oktoba 28, 2005.
Mwaka 2007, ilibadilishwa jina kutoka Mzizima na kuwa Azam SC kabla ya mwaka 2008 kutambulika rasmi kama Azam FC.
Wababe hao wa Chamazi wenye maskani yao Azam Complex, kihistoria wamefanikiwa kutwaa mataji tofauti mara 10, ikibeba ubingwa wa Ligi Kuu mara moja, Kombe la Kagame (2), Kombe la FA (1), Ngao ya Jamii (1) na Kombe la Mapinduzi (5).
Msimu huu hadi sasa, Azam FC iko moto ikiwa ndio kinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikishinda mechi zote tano ilizocheza na kujikusanyia jumla ya pointi 15 kileleni. 
Pia unaweza kuifuatilia azam fc kupitia akaunti zake za Instagram za azamfcofficial na azamfccommunity