Home Mchanganyiko UFUNGUZI WA JENGO LA “MICHENZANI MALL” MJINI ZANZIBAR

UFUNGUZI WA JENGO LA “MICHENZANI MALL” MJINI ZANZIBAR

0

BAADHI ya Wananchi wa Zanzibar wakifuatilia hutuba ya
Ufunguzi wa Jengo jipya la Maduka ya Kisasa la Michezani Mall
lililojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, wakati Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
(hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo iliofanyika katika 
viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.
Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa jukwaa kuu wakifurahia wakati 
wasoma Utenzi Amina Mkombe akisoma utenzi katika hafla hiyo iliofanyika
katika viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge Michezani Jijini Zanzibar,
(kushoto kwa Rais)Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Balozi Mohammed Ramia
Adbiwawa na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi na (kulia kwa
Rais ) Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF Dkt. Suleiman Raishid Mohammed  na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na
Ikulu)

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis
Mussa akizungumza na kutowa maelezo ya Kitaalam ya Mradi wa ZSSF wa
Ujenzi wa jengo jipya la Maduka ya Kisasa Michezani Mall, wakati wa
hafla hiyo ya ufunguzi wake uliofanyika leo 5/10/2020.(Picha na Ikulu)WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia
Abdiwawa akizungumza katika ufunguzi wa jengo jipya la Maduka ya Kisasa
la Michezani Mall wakati ya hafla ya ufunguzi huo uliofanyika leo katika
viwanja vya Mapinduzi Square Kisombe michezani Jijini Zanzibar.(Picha na
Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) akiwa mgeni rasmi akijumuika na Viongozi mbali mbali katika kulifunguwa Jengo la Zanzibar Mall Michenzani Mjini Zanzibar hafla iliyofanyika leo.[Picha na Ikulu].05/10/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika Ufunguzi wa  Jengo la Zanzibar Mall Michenzani Mjini Zanzibar lililojengwa na Kampuni ya  CREJ kutoka Nchini China hafla iliyofanyika leo viwanja vya Mapinduzi Squre Michenzani.[Picha na Ikulu].05/10/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) akiwa mgeni rasmi akijumuika na Viongozi mbali mbali alipokata utepe kulifunguwa Jengo la Zanzibar Mall Michenzani Mjini Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Mapinduzi Squre Michenzani.[Picha na Ikulu].05/10/2020. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akifuatana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF Nd,Nasra Issa Machano pamoja na Viongozi wenginei alipotembelea sehemu mbali mbali za  Jengo la Zanzibar Mall Michenzani Mjini Zanzibar mara baada ya kulifungua rasmi,hafla iliyofanyika leo  Michenzani Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu].05/10/2020.