Home Mchanganyiko MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI TAREHE 29/09/2020

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI TAREHE 29/09/2020

0

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Wilaya ya Kinondoni katika kuadhimisha siku ya Moyo Duniani tutafanya  upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani. Upimaji huo utaenda sambamba  na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Upimaji  utafanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers vilivyopo Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kufanya upimaji kwa watoto na watu wazima.  Wananchi watapimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na  kupewa ushauri. Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu. Kauli mbiu: “Maamuzi sahihi kwa afya bora ya moyo”.

 

Wafanyakazi wa Taasisi hii tunahakikisha tunatoa huduma bora zaidi za magonjwa ya moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo. Mpango wetu ni  kutoa tiba ya moyo,  upasuaji wa moyo na elimu kwa jamii ambayo itawasaidia wananchi kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Tunawaomba wananchi muadhimishe siku hii kwa kujitokeza  kwa wingi kupima afya zenu hii itawasaidia kujua kama mna matatizo ya moyo au la na hivyo kuanza matibabu mapema kwani asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea katika Taasisi yetu mioyo yao haiko katika hali nzuri.