Home Mchanganyiko VIONGOZI WAKUU WA WIZARA TATU WATEMBELEA BANDA LA STAMICO

VIONGOZI WAKUU WA WIZARA TATU WATEMBELEA BANDA LA STAMICO

0

………………………………………………………………………………

 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetembelewa na viongozi wakuu kutoka wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe, Naibu Katibu Mkuu Bw. Ludovick Nduhiye, pamoja na Katibu Mkuu WIzara ya Madini Prof. Simon Msanjila na kufaurahishwa na utendaji bora wa STAMICO.

Akiongea wakiwa katika banda la STAMICO Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema amefurahishwa kuona STAMICO na kasi ya STAMICO katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa niaba ya Serikali.

Aidha alifurahishwa jinsi Shirika linavyotoa huduma bora na za kitaalamu za uchorongaji kwa njia za kisasa.
Ameitaka STAMICO kuifikisha huduma ya uchorongaji kwa wachimbaji wadogo kwani wameshaonesha nia na uhitaji wa huduma hiii katika kuboresha shughuli za uchimbaji katika maeneo yao.

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Makatibu Wakuu hao na kuelezea namna Shirika linavyotekeleza dhana nzima ya ushiriki na ushirikishwaji wa watanzania katika sekta madini (Local content) kupitia kampuni yake tanzu ya STAMIGOLD.

Aidha ameleza namna ambavyo STAMICO inavyotumia maonesho haya kuwaelimisha wachimbaji hasa wadogo na kupokea maoni yao ili kuboresha njia mbalimbali za kuwasaidia sambamba na kutatua kwa Pamoja changamoto zinazowakabili.

Makatibu Wakuu hao wametoa with STAMICO kuendelea kuchapa kazi kwa bidiii na uaminifu.