Home Michezo BAYERN MUNICH YAICHAPA 2-1 SEVILLA NA KUTWAA TAJI LA SUPER CUP

BAYERN MUNICH YAICHAPA 2-1 SEVILLA NA KUTWAA TAJI LA SUPER CUP

0

Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia na taji la UEFA Super Cup baada ya ushindi wa 2-1 dhid- ya Sevilla usiku wa jana Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest, Hungary. 

Sevilla ilitangulia kwa bao la Lucas Ocampos dakika ya 13 kwa penalti baada ya Ivan Rakitic kuangushwa kwenye boksi, lakini Leon Goretzka akaisawazishia Bayern Munich dakika ya 34, kabla ya bao la Robert Lewandowski kukataliwa na mchezo ukaisha 1-1 ndani ya dakika 90.

Katika dakika 30 za nyongeza ndipo mtokea benchi, Javi Martinez akaifungia bao la ushindi Bayern Munich dakika ya 104, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wakiwaangusha mabingwa wa Europa League mbele ya mashabiki 20,000 kwenye Uwanja unaochukua watazamaji 67,000, kati yao 500 wakisafiri kutoka Hispania na 1,000 kutoka Ujerumani PCHA ZAD SOMA HAPA