Home Mchanganyiko UMMY MWALIMU KUANZISHA UJENZI WA HOSTELI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI...

UMMY MWALIMU KUANZISHA UJENZI WA HOSTELI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI JIJINI TANGA

0

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa
Kata ya Mzizima Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimnadi mgombea
udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakati wa mkutano wake wa
kampeni
Mgombea
udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba kushoto akimuombea kura
mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa
mkutano wake wa kampeni
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na mgombea
udiwani wa kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakifuatilia matukio
mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
Msanii Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo

Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa
Jimbo hilo atahakikisha anajitahidi kuanzisha ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi wanaosoma
shule za sekondari wanaokaa mbali ili kuwawezesha kusoma bila uwepo wa
vikwazo.

Hatua
hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari kukaa mbali
na maeneo ya shule hali inayopelekea kushindwa kufika  kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri.

Ummy
aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima katika uwanja
wa Gogovivu kwenye mkutano wake wa kampeni ambapo alisema suala hilo litakuwa
mwarobaini wa kuwaepusha wanafunzi kutokufika shuleni.

 “Ninaamini
ujenzi wa Hostel utasaidia kupunguza changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi
wanaosoma shule za mbali kutokana na kukosekana kwa usafiri kwa baadhi ya
maeneo wanayokwenda”Alisema

Hata
hivyo alisema kwamba ataendelea pia kushirikiana nao  kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba
vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

“Ninafahamu
shule za msingi Mafuriko,amboni,rubawa na mleni kuna maadhibi miomdnboni sio
mizuri na madarasa hayatoshi,ninawaomba sana ..mchango wangu niliiutoa kabla
sijawa mbunge niaminini niweze kushirikiana nanyi kuboresha elimu hasa
miundombinu na kutafuta madawati kwa ajili ya wanafunzi”Alisema Ummy

“Lakini
pia sijaisahau shule ya sekondari Kiomoni nimewekeza ujenzi wa madarasa mawili
ninawaomba sana mnichague ili tuweze kuiboresha zaidi”Alisema

Hata
hivyo alisema pia atalazimika kubadilisha jina la shule ya sekondari Kiomoni
kwa sababu ni ya shule ya kata ya Mzizima hivyo watabadilisha jina liweze kuwa
shule ya sekondari Mzizima.

 

“Niaminini
tuweze kutatua changamoto za wanafunzi wa Rubawa,Mleni  ambao wanakwenda mpaka sekondari ya kiomoni
kwa  usafiri wenye changamoto na
kupelekea kushindwa kufika shuleni kwa wakati”Alisema