Home Mchanganyiko BILIONI 100 KUMALIZA TATIZO SUGU LA MAJI KATIKA WILAYA NNE MKOANI TANGA

BILIONI 100 KUMALIZA TATIZO SUGU LA MAJI KATIKA WILAYA NNE MKOANI TANGA

0

MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati alipotembelea
mradi wa Maji Michokeni wilayani Pangani wakati wa ziara yake kulia ni
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah

MKUU
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara
hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

MKUU
wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na katikati ni Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo

MSIMAMIZI
wa Mradi wa Maji unatoa Maji kutoka Pongwe hadi Muheza Adela Mboya
akielezea jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
wakati wa ziara yake

Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza wakati wa
ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alipotembelea mradi wa
maji Pongwe unaopeleka maji wilayani Muheza

TATIZO sugu la uhaba wa maji katika wilaya nne za mkoani
Tanga linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kufuatia Serikali kuwa na
mpango wa kutekeleza mradi mkubwa utakaogharimu sh 100. bilioni.


Wilaya zitakazonufaika na mradi huo utakaotoa maji katika mto Pangani ni Pangani,Muheza,Korogwe na Handeni.

 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema hayo wakati wa
ziara yake yakukagua miradi ya maji inayosimaniwa na Mamlaka ya maji na
usafi wa mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA katika wilaya ya Muheza
mkoani Tanga.

 

Amesema Kuwa ujio wa miradi hiyo katika mkoa huo utaweza
kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia
90% hali ambayo itasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi.

 

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo amesema kuwa hali
ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa maeneo ya Vijiji ni asilimia 65%
wakati katika maeneo ya mjini ni asilimia 18%pekee.

 

Amesema kuwa ukamilikaji  wa miradi ya maji utaweza
kuongeza kiwango cha huduma hiyo hadi kufikia asilimia 52% na hivyo
kusaidia kupunguza kwa kiasi fulani Changamoto ya ukosefu wa maji katika
wilaya hiyo.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa
mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA Geofrey Hilly amesema kuwa
kukamilika kwa mradi wa maji kutoka Pongwe kwenda Muheza kutasaidia
huduma ya maji hadi katika Vijiji vya jirani katika  maeneo ambayo
mabomba ya maji yatapita.