Home Mchanganyiko WAZEE MAGU WAAHIDI KURA KWA JPM DC AKISHUSHA NEEMA KWAO

WAZEE MAGU WAAHIDI KURA KWA JPM DC AKISHUSHA NEEMA KWAO

0

Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli, akicheza ngoma na akina mama wazee wa Kata ya Nkungulu Tarafa ya Ndagalu jana alipokwenda kuzungumza na wazee wa kata hiyo ili kufahamua changamoto na kero zao ili zitafutiwe ufumbuzi.

Wazee wa Kata ya Nkulungu katika Tarafa ya Ndagalu Wilayani Magu wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Salum Kalli.

Mzee Kilala Masasila (105) akipokea fedha ya kujikimu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, jana baada ya kufanya ziara na kuzungumza na wazee wa kata ya Kabila wilayani humo.Picha zote na Baltazar Mashaka
………………………………………………………………….

NA BALTAZAR MASHAKA, Magu

WAZEE wa kata mbalimbali wilayani Magu wameahidi kumpigia kura za heshima mgombea Urais wa CCM, Rais John Magufuli kutokana na kazi alizofanya za maendeleo.

Wamesema hawatapotea njia wala kudanganyika na sera za vyama vya siasa visivyoaminika ili kuonyesha ukomavu wa CCM wa kuleta maendeleo watampigia kura Rais Magufuli, wabunge na madiwani kwenye Jimbo la Magu.

Walitoa kauli hiyo jana mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, baada na kuzungumza na wazee wa kata za Jinjimili, Kabila,Gh’haya, Nkungulu katika Tarafa ya Ndagalu.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, Thabitha Yakob mkazi wa Kijiji cha Mwashepi, alisema Rais Magufuli amewafanyia mengi yakiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya na hospitali hivyo Oktoba 28, mwaka huu hawatamuangusha.

“Kwa aliyotufanyia Rais Magufuli hatukustahili kufanya uchaguzi lkini kwa kuwa ni utaratibu tunaomba aendelee  kuongoza kwa miaka mingi na kwa kuthibitisha hilo Oktoba 28, tutampigia kura za kishindo yeye , mbunge na madiwani,kazi alizofanya ni kubwa,”alisema Yakob. 

Aidha Evarist Didas  alisema wanampongeza Mkuu wa Wilaya kwa uchapakazi, ukaribu wake kwa wananchi na kuwa hawajawahi kuona DC  anayehangaika vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua

“Ni kiongozi wa mfano ingawa wamepita wengi Magu yeye amewapita, kwa muda mfupi ametembelea vijiji vyote 82 na kata 25, kila mara yuko vijijini kuwasilikiza wananchi,hajifungii ofisini.Pia ni Rais Magufuli ni Nabii, ingewezekana aingeizwa kwenye Biblia kwa vile haiwezekani Watanzania wampigie kura za ndiyo aendelee kuwatumikia wanyonge,”alisema Didas.

Kwa upande wake Kalli alisema wazee ni lulu ya taifa, wanastahili heshima na kuthaminiwa, ili waendelee kupata heshima hiyo Oktoba 28, wasipotee bali wamchague Rais Dk.Magufuli anayeishi na shida za wazee na kuzitatua ili waishi kwa usalama na kunufaika kwa rasilimali za nchi na kufaidi matunda ya uhuru walioupigania.

Alisema maendeleo yote yanayoonekana yameletwa na serikali ya CCM chini ya chini ya Rais Mafuguli ,  anajenga reli ya kisasa (SGR),Bwawa la Nyerere la kufua umeme, Daraja la Kigongo-Busisi na pia barabara za Magu-Mahaha-Shishani hadi Bariadi na  barabara ya Magu-Kwimba zitajengwa kwa kiwango cha lami, zote ziko kwenye ilani ya CCM.

“Anafahamu jinsi wazee mlivyohaingaika kupigania uhuru wa taifa hili, asitokee mtu wa kuwazunguka, wengine wanaomtukana hakuna walichowahi kukifanya cha maendeleo ,hivyo maendeleo hayo mmeyawezesha ninyi wazee, vijana hawakuwepo na hawajui uchungu wa nchi hii mliona nao hivyo msigawanyike muwezesheni Rais Magufuli kupata kura za kishindo,”alisema Kalli.

Akizungumzia mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) kaya ama wanufaika baada ya uchaguzi mkuu, wataalamu watapita kwenye vijijini vyote kuwabaini waliosahaulika na kuingizwa kwenye mpango huo.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Magu pia alitoa msamaha kwa wazee wenye miaka zaidi ya 60 watakaofiwa wenzi wao wakiwa wamelazwa hospitali ama vituo vya afya, wasitozwe gharama za kuhifadhi miili ya marehemu atalipa gharama hizo yeye (mkuu wa wilaya) na kusistiza wazee wataendelea kutibiwa bure na kuonya watumishi wa afya wanaowakejeli na kuwatolea lugha chafu, waaeche tabia hiyo.