Home Mchanganyiko SAO HILL WAWAPIGA MSASA WATENDAJI WA KATA NA TARAFA KUKABILIANA NA JANGA...

SAO HILL WAWAPIGA MSASA WATENDAJI WA KATA NA TARAFA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO KWENYE MISITU

0

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamnhuri Wiliam akitoa majizo kwa watendaji wa wilaya hiyo kuzingatia mafunzo waliyopewa juu ya kukabiliana na janga la moto

Picha ya pamoja ya baadhi ya watendaji wa wilaya ya Mufindi na Viongozi kutoka shamba la miti Sao Hill

Afisa zimamoto akitoa elimu kwa watendaji juu ya madhara ya moto katika msitu wa Sao Hill

Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Wakala wa misitu Tanzania TFS kupitia
shamba la Sao hill na Serikali ya Wilaya ya Mufindi wameanza kutoa elimu kwa
maafisa watendaji wa kata na Tarafa juu ya ulinzi wa maeneo ya msitu na hasa
juu ya kukabiliana na janga la moto unaozuka kutokana na shughuli za kibinaadam
na kuteketeza msitu kila mwaka.
 

Akizungumza wakati Warsha maalum kwa
ajili ya kukabiliana na moto inayoteketeza misitu katika wilaya ya Mufindi,
Mhifadhi mkuu wa
Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema kuwa lengo la mafunzo
hayo ni kuwaongezea viongozi uwezo wa elimu ya kukabiliana na janga la moto

“Kulingana na hasara inayojitokeza
mara kwa mara awamu hii Wakala wa misitu Tanzania TFS pamoja na Serikali
wameona ni vyema kuweka msisitizo katika kuwajengea uwezo watendaji wa kata na
tarafa juu mbinu shirikishi za tahadhari ya kuzuka kwa mioto na namna ya
kukabiliana nayo ili kuunusuru msitu wa sao hill na mashamba ya miti ya
wananchi  wilayani Mufindi” alisema
Mwita 

Mwita alisema kuwa mpango wa elimu
shirikishi kwa viongozi na wananchi ni endelevu na wanataraji kupata matokeo
chanya kutokana na mikakati iliyopo kwa viongozi hao kwenda kwa wananchi
wanaowaongoza.
 

Aidha Mwita alisema kuwa Kando ya
moto unaoteketeza misitu kila mwaka uvamizi katika maeneo ya shamba la miti la
serikali sao hill ni changamoto nyingine ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi ili
kumaliza kabisa changamoto hizo.
 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mufindi Jamnhuri Wiliam ametoa siku kumi na nne kwa maafisa tarafa ya Malangali
na Saadani kuwasilisha ofisini kwake taarifa ya bank Ardhi iliyopo katika
maeneo yao ili kuwapatia wananchi waliondoka katika maeneo vamizi ya hifadhi ya
msitu wa Sao hill.
 

Jamhuri William ametoa agizo hilo
kufuatia wananchi zaidi ya 60 waliovamia msitu huo kuridhia takwa la kuyaachia
maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuyatunza maeneo ya
hifadhi ya msitu huo unaotajwa kuchangia pakubwa ukuaji wa uchumi wa wilaya
hiyo pamoja na pato la Taifa.
 

Jamhuri alitumia Warsha hiyo kueleza
hatari ya moto inavyoweza kudumaza maendeleo yatokanayo na misitu
 

Hata hivyo ameonesha kutofurahishwa
na maagizo aliyoyatoa dhidi ya afisa tarafa ya malangali juu ya benki ardhi ili
kuwapatia wananchi waliovamia ardhi iliyo chini ya hifadhi ya msitu wa Sao hill
na sasa anatoa maagizo
 

Msitu wa kupandwa wa sao hill ulio
mkubwa kuliko yote afrika mashariki kando ya kuchangia pato la taifa umekuwa
mhimili wa uchumi wa wilaya ya mufindi ukifungua fursa ya ajira kwa wananchi
kuajiriwa katika kazi za uhifadhi lakini pia umefungua fursa kubwa ya kiuchumi
kwa wananchi kujihusisha na kilimo pamoja na biashara ya mazao ya misitu