Home Mchanganyiko DKT MABULA: ‘TUTATENGENEZA BARABARA YA AIRPORT-KAYENZE KWA KIWANGO CHA LAMI’

DKT MABULA: ‘TUTATENGENEZA BARABARA YA AIRPORT-KAYENZE KWA KIWANGO CHA LAMI’

0

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia CCM Dkt Angeline Mabula ameahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha barabara ya kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kupitia Kayenze inajengwa na kukamilika kwa kiwango cha Lami.

Dkt Mabula ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bugogwa jijini Mwanza, Ambapo amesema kuwa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka wa 2020-2025 imeahidi ujenzi wa barabara hiyo itakayokuwa na urefu wa kilomita 46.3 hivyo kuwaomba wananchi hao kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo

‘.. Ukiisoma vizuri Ilani yetu ya Uchaguzi imeitaja barabara hii kuwa itejengwa kwa kiwango cha Lami, Na bahati nzuri upembuzi yakinifu umeshaanza ili barabara yetu iweze kujengwa, Ninachowaomba tupeni kura za ndio oktoba 28, ili Mimi, Mhe Rais Magufuli na Diwani tukashirikiane kukamilisha mradi huu ..’ Alisema

Akimkaribisha Mbunge huyo, Meneja Kampeni wa Jimbo la Ilemela Ndugu Kazungu Safari Idebe akataja miradi mbalimbali  iliyotekelezwa ndani ya kata hiyo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya mbunge huyo ikiwemo ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugogwa, Ununuzi wa kompyuta zaidi ya 20 kwa shule ya sekondari Bugogwa, Ujenzi wa sekondari mpya ya Kisundi, ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Igogwe, ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya kutolea huduma uliogharimu zaidi ya milioni mia nne kutoka Serikali kuu kwa kituo cha afya Karume.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akawaomba wananchi hao kuendelea kukiamini chama chake na kukipa kura za ushindi siku ya uchaguzi mkuu kwa nafasi ya Urais, ubunge na udiwani ili miradi ya maendeleo iliyokuwa ikiendelea kutekelezwa iweze kukamilika kwani kila walichoahidi katika uchaguzi uliopita kimekamilika.