Home Siasa Wanaokosa cha kuwaambia wanananchi wanaitukana serikali

Wanaokosa cha kuwaambia wanananchi wanaitukana serikali

0

KAMPENI za uchaguzi mkuu mara nyingi zinagubikwq na vioja vya hapa na pale. Vinaweza kukupoteza au kukurudisha kwenye njia.

Hata hivyo, imekuwa ni desturi kwa nchi zinazoendelea kuchukulia suala la uongozi kama tunu inayotakiwa kuchukuliwa na kila mtu hata kama hana uwezo.

Wakati fulani Mwalimu Julius Nyerere wakati akimnadi mgombea urais Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Benjamin Mkapa aliona vituko hivyo hata akajiuliza ikulu kuna nini mbona watu wanapakimbilia sana.

Haiyumkiniki kila mmoja anataka kuwa rais walau kwa siku moja. Ana lengo jema la kuibadili Tanzania au anataka kukinufaisha chama chake na zaidi ni yeye binafsi.

Nimefuatilia kampeni za mwaka huu. Nilichobaini bado vyama vya upinzani vina safari ndefu yenye milima na mabonde. Bado kuna kutoelewana juu ya msingi wa hoja wanazojenga.

Ukimsikiliza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli, utaona anatumia muda mwingi kuwaeleza wananchi mambo aliyoyafanya kupitia ilani ya chama chake aliyokabidhiwa kuisimamia miaka mitano iliyopita.

Anaeleza kipi aliahidi akatimiza na kipi aliahidi akashindwa kutimiza na kwanini alishindwa, je ana maelezo au mipango gani kwa miaka mitano ijayo ikowa wananchi watampa nchi kwa mara ya pili.

Ukimsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Benard Membe unaweza kujiuliza hiki ninachokisikia kinatoka kinywani kwa mtu anayejulikana kwa hekima zake na kuaminiwa na wananchi.

Mathalan akiwa Kilwa alipata kusema: “Mkinipa urais nitahakikisha naiinua Kanda ya Kusini hasa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuwa mmesahauliwa sana. Barabara mbovu na huduma zote zinapelekwa katika mikoa mingine nyinyi mmesahauli.”

Hii ni kauli ya kibaguzi iliyojaa uongo. Mikoa ya Kusini kwa muda mrefu haikuwa na barabara ya uhakika. Sasa hivi kila mtu anajua serikali ilifanya nini kujenga barabara inayounganisha Mkoa wa Pwani na ukanda huo.

Daraja la Mkapa kila mmoja anajua namna lilivyounganisha uchumi wa mikoa ya kuaini. Kama hiyo haitoshi kuna upanuzi wa Bamdari ya Mtwara ili kuiongezea uwezo wa kuegesha meli kuwa.

Lakini Membe ambaye alikuwa serikalini kwa miaka zaidi ya 20 anasahau kabisa suala la maendeleo yaliyopelekwa kwenye mikoa hiyo pia anasahau kuwa maendeleo hayana ukanda. Hiyo ni ishara ya ubaguzi na ukabila.

Mfano mwingine Membe anasema akipewa madaraka atarejesha kangomba. Huu ni mfumo unaotumiwa na wenye fedha kuwadhulumu wakulima wa korosho. Wanaweka fedha wakati korosho zikiwa maua kabisa.

Kisha wanawayangulizia fedha kidogo wakulima, wakati wa mavuno ukifika wakulima wanashika tama wakati mazao yakichukuliwa na kuuzwa kwa bei ya kulangua. Matokeo yake mkulima anapata fedha kiduchu huku laghai ambaye hajashika jembe wala kupulizia dawa mmea anapata fedha nyingi.

Kama hiyo haitoshi mgombea huyo huyo anasema akipewa ridhaa ya kuongoza nchi ataondoa utaratibu wa wavuvi kuzuiwa kutumia nyavu zenye matundu madogo.

Maana yake anakwenda kuruhusu uharamia wa kumaliza mazalia ya samaki kwa wavuvi kuendelea kutumia nyavu zenye matundu madogo maarufu makokoro.

Hii haiko sawa, wananchi hawapaswi kulaghaiwa kwa ahadi zisizoweza kutimia. Ahadi ambazo ni wazi zinalenga kuvuruga utaratibu wa nchi.