Home Michezo KLABU YA SIMBA IMEMTEUA BARBARA KUMRITHI SENZO

KLABU YA SIMBA IMEMTEUA BARBARA KUMRITHI SENZO

0

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imemteua Barbara Gonzalez kuwa mtendaji mkuu CEO mpya wa klabu hiyo baada aliyekuwa ameshika nafasi hiyo Senzo Mbatha kutimkia kwa maasimu wao Yanga hivi karibuni

Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa ni makubaliano ya uongozi jana ambapo walikuwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi, Septemba 4.

Barbara anakuwa CEO wa kwanza wa kike katika klabu za ligi kuu Tanzania bara na kuiongoza klabu kubwa kama Simba.