Home Siasa WANANCHI WANAJUA KUCHAMBUA PUMBA NA MCHELE, WAPO WAGOMBEA VIONGOZI NA WANAHARAKATI

WANANCHI WANAJUA KUCHAMBUA PUMBA NA MCHELE, WAPO WAGOMBEA VIONGOZI NA WANAHARAKATI

0

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli akizungumzakatikamkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM mwishoni mwa wiki.

…………………………………………

Na Mwandishi Wetu

KAMPENI za uchaguzi mkuu mwaka 2020 zimeanza kwa kishindo, mambo yanayofanyika ni dhahiri watakaoamua kwenye sanduku la kura ni wale waliopata wasaa wa kuwasilikiliza wagombea walau kwa uchache.

Hta hivyo, lipo tatizo limejitokeza la kutoa vioja badala ya hoja kwa kila kampeni kulingana na tabia, hulka na mwonekano wa chama au mgombea.

Mathalan, mgombea wa Chama cha Chauma Mzee wetu Hashim Rungwe Spunda hii ni mara ya pili anagombea nafasi ya urais kupitia chama chake, lakini vituko anavyovionyesha ni dhahiri analenga kufurahisha wananchi badala ya kutaka kura zao.

Mgombea wa Chama cha ACT Wazlendo Bernald Membe.

……………………………………….

Anasema kampeni zake zitakua na ‘ubwabwa,’ watu kabla ya kusikiliza atahakikisha matumbo yao yamejaa chakula cha kutosha. Tena wali kwa kuku.

Kilichotokea kwa hoja hii ni kugeuzwa kituko katika mitandao ya kijamii. Kila mmoja mwenye uwezo wa kutengeneza kituko anachokijua basi anafanya hivyo.

Tukimuangalia Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), ni kama amepoteza dira. Si Yule Profesa Lipumba wa kupita kila mahali akashangiliwa, si Profesa Lipumba wa kuzua taharuki hata watu wakapigwa mabomu ya machozi kwa hamaki.

Mgombea wa Chama cha Chadema Tundu Lissu.

…………………………………….

Hadi sasa kampeni zimetimiza wiki ya kwanza tangu zilipozinduliwa Agosti 26, 2020 lakini sera za CUF hazijulikani. Bado haijajulikana chama hicho kimeingia kwenye kinyang’anyiro cha kampeni kwa lengo gani.

Aidha, ukimtazama mtu kama Tundu Lissu wa Chadema. Yeye hoja zake ni za matusi. Tangu alipowasili nchini akitokea Ubelgiji kwenye matibabu hajaweza kuzungumza hata sentesi moja iliyonyooka inayoonesha maana yoyote kwa jamii.

Zaidi watu waliomsindikiza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake pale Mbagala Zakhiem, akiwemo mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema waliishia kuzungumza hoja za kubumba ikiwemo kumtusi Rais Dk. John Magufuli pamoja na kulinajisi jina la Ikulu takatifu kwa kuiita ‘Getto’ yaani makazi ya wahuni.

Kiufupi hadi wananchi wanandoka katika eneo lile sijui kama kuna chochote cha maana walichookota, zaidi ya kusema wanataka mabadiliko. Haijulikani ni mbadiliko ya aina gani wanayoyataka kwa sababu tayari Serikali ya Awamu ya Tano imeshafanya mambo makubwa yaliyoacha gumzo duniani.

 

Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.

……………………………………..

Mwisho wa yote Lissu akaishia kusifia sehemu ya kazi hizo ikiwemo madaraja ya Dar es  Salaam yatakayosadia kupunguza msongamano wa magari.

Huyu ndiye anayejiita mpinzani mkuu wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Itakumbukwa Dk. Magufuli wakati wa uzinduzi wa kampeni zake siku ya Jumamosi, Agosti 29 mwaka huu pale Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma alitumia saa mbili kwanza kueleza yale aliyoyatekeleza baada ya kuomba ridhaa ya kuongoza nchi miaka mitano iliyopita, lakini pia kuwaomba tena wananchi kuwa anataka kumalizia kile alichokiacha.

Walau mtu namna hii mnaweza kukaa meza moja mkazungumza, mkaelewana lugha na kujua nini cha kufanya. Kwa sababu anakueleza habari ambazo zinaonekana, ni dhahiri anaweza kuzitekeleza na zikakamilika.

Mfano alizungumzia masuala ya maji, afya, elimu, nishati, kilimo na ongezeko la ajira ka kutumia sekta za kimkakati. Zadi ya yote akaahidi kumalizia vijiji vilivyobakia ambavyo havina umeme.

Mambo haya yanaonekana, kuna vitu amevizungumza ikiwemo ujenzi wa mitambo ya kufua umeme wa maji Megawati 2115, kitu kinachoshikika. Kitu kinachoendelea na fedha zipo. Mradi wa reli ya kisasa (SGR),ni kitu kinachoshikika, kipo na kazi inaendelea.

Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo  Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kulia ni Mgombea wa Chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba.

…………………………………………

Nilichotaraji, ni kuona wagombea anabishana kwa hoja. Wanajaribu kumpinga kwa hoja mgombea wa CCM ambaye anataka ridhaa ya wananchi kwenda kumalizia alichokianza nasi kumtusi au kutaja taja majina ya watu bila utaratibu wala nidhamu.

Mgombea wa ACT Wazalendo, Benard Membe amefunikwa na mfumo wa chama ambacho ni kipya kwake hana hata miezi sita tangu ajiunge katikati ya mwaka huu.

Hajui anataka nini wala hajui chama chake kinahitaji nini. Amefilisiwa hoja matokeo yake anaishia kuzunguka zunguka bila kusema kile chenye kuonekana.

Kwa kifupi, uchaguzi wa mwaka huu utakua wa upande mmoja kwa sababu wananchi si wajinga. Wanajua kuchagua pumba na mchele