Home Siasa Wana CCM Osunyai wapewa somo

Wana CCM Osunyai wapewa somo

0

Wanachama na waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika kata ya osunyai jijini Arusha wameaswa kutekeleza kwa vitendo ahadi mbalimbali za chama hicho lakini pia kumuunga mkono raisi magufuli kwa njia ya utekelezaji wa miradi mbalimbali

Kwa sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hususani kwa mkoa wa arusha kimefanikiwa kutekeleza ahadi mbalimbali za kijamii lakini ili ahadi hizo ziendelee kuwanufaisha wananchi lazima kila mteule wa wananchi  ahakikishe anafuata nyayo za raisi magufuli

Hayo yameelezwa wiki iliyopitana bw Christopher Salvatory  ambaye ni mgombea mteule wa udiwani kata ya osunyai jijini Arusha wakati akiongea na maelfu ya wananchi wa kata hiyo ambao walikusanyika katika ofisi ya kata ya chama hicho kwa malengo ya kumsindikiza kuchukua fomu rasmi ya udiwani wa kata hiyo

Christopher alisema kuwa kwa kipibdi ambacho raisi magufuli ameongoza ameonesha nuru kubwa sana kwa wananchi kwa kuwa ameweza kutatua changamoto ambazo zilikuwa ni sugu

Amefafanua kuwa kwa kupitia nuru na uwajibikaji wa raisi magufuli ni wazi kuwa kila mgombea ambaye anawkilisha chama cha mapinduzi anatakiwa kuiga mfano lakini punde atakapochaguliwa basi atekelezs na kusimamia wananchi

” Raisi wetu ameonesha uzalendo mkubwa sana lakibi sisi kama wadau tunatakiwa kuhakikisha kuwa kwa kipindi hiki tunamuunga mkono lakini pia uwajibikaji na usimamizi wa miradi mbalimbali na hii itasaidia wananchi wetu ambao bado wanakabiliwa na changamoto lukuki”aliongeza

Katika hatua nyingine mgombea huyo alisema kuwa ccm imempa heshima kubwa sana ya kuweza kupeperusha bendera ya kata hiyo ya Osunyai lakini pia ana mpango wa kuhakikisha kuwa anatatua changamoto zikiwemo za miundombinu imara ndani ya kata hiyo

Alihitimisha kwa kuwataka wana ccm kuwa kitu kimoja na kuweza kutafuta kura kwa kishindo za wagombea kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge,hadi uraisi