Home Mchanganyiko TEF YAWAONYA WANASIASA WATAKAOTUMIA LUGHA ZA MATUSI KATIKA KAMPENI ZAO

TEF YAWAONYA WANASIASA WATAKAOTUMIA LUGHA ZA MATUSI KATIKA KAMPENI ZAO

0

KAIMU Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile akizungumza na waadndishi wa Habari Jijini Dodoma.Baadhi ya waandishi wa habari Jijini Dodoma wakimsikiliza KAIMU Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile(hayupo pichani).

……………………………………………………………….

Na. Alex Sonna, Dodoma

KAIMU Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile amesema vyombo vya habari havitatumia habari za wagombea wanaotoa matusi majukwaani na vitatoa nafasi sawa katika kampeni za kuwanadi wagombea watakaoeleza Sera zao katika kuwaeletea wananchi maendeleo

Hayo yamebainshwa  wakati akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dodoma .

Balile aamesema kuwa wagombea wote wana haki sawa ya kupata nafasi kwenye vyombo vya habari lakini havitakuwa tayari kutoa habari zilizojaa matusi.

 Kauli hiyo ya Balile inatolewa  baada ya  kauli ya mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia Chadema Mchungaji Peter Msigwa wakati wa kumtambulisha mgombea urais wa chama hicho Tundu Lissu hivi karibuni  akiwataka wafuasi wa chama hicho kususia vyombo vya habari kwani havitoi habari zao.

” TEF tulijadili suala hili na tukaona tusipolitolea tamko litaleta athari kwa waandishi katika kampeni za uchaguzi,tuna historia ya waandishi kuumizwa katika uchaguzi ,kwa tumeona tukiliacha hili bila kulikemea Siku nyingine anaweza kuhamasisha waandishi wapigwe.” Ameeleza Balile.

Balile amesisitiza kuwa vyombo vya habari havipo kupigwa maana vyombo haviwezeshi  chama cha siasa kishinde.

Katika hatua nyingine ametumia fursa hiyo kuviomba vyama vyoye vya siasa kufanya siasa zao kwa kueleza Sera na siyo kuhamasisha vurugu dhidi ya waandishi wa habari.

“Hivyo tusiwachochee wananchi kupambana na wanahabari ,sisi tupo hapa kufanya kazi kwa usawa na vyama vyote”, amesisitiza Balile.