Home Michezo Waziri Mwakyembe “Tuna Mpango wa Kuboresha Sekta ya Michezo “

Waziri Mwakyembe “Tuna Mpango wa Kuboresha Sekta ya Michezo “

0

………………………………………………..

Na Joctan Myefu 

NJOMBE, Waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo Dr Harison Mwakyembe amesema mafanikio makubwa ambayo wachezaji wa kitanzania wameyapata kwa kucheza soka na michezo mingine nje ya nchi kuisukuma serikali kuanza kuboresha miundombinu ya michezo ili kuzalisha zaidi vipaji vitakavyoenda nje ya nchi na kuleta fedha za kigeni nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ziara yake mkoani Njombe waziri mwakenyembe Amesema serikali imeanza mpango wa kuboresha viwanja na kujenga shule za mpira na michezo mingine ili kutengeza akina samata na kevini John wakutosha.

Alipohojiwa kuhusu mwenendo wa mgogoro wa msakata kabumbu kutoka Nchini Ghana Benad Morison na waajiri wake wake wa zamani Dar Young African Waziri Mwakyembe amegoma kulizungumzia kwa kina kwa madai ya kwamba bado lipo katika vyombo vya maamuzi huku akionyesha kufurahishwa na mwenendo wa kikosi cha wekundu wa msimbazi simba na kuwataka kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Nae mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Mwita Rubirya akizungumzia mwenendo na mipango ya mkoa kwenye soka amesema upo mkakati wa kujenga uwanja wa kisasa wenye nyasi bandia ili kukuza  soka ambalo ajira kwa sasa.